August 3, 2020

MRISHO Ngassa kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amewaaga rasmi mashabiki wake kwa kusema kuwa msimu ujao hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga.

Kupitia ukurasa wa Instagram,Ngassa ameandakika hivi:-"Kwanza nitoe shukrani zangu kwa wote tuliokuwa pamoja katika kipindi chote, Yanga viongozi wangu mashabiki na wachezaji wenzangu kwa kikao kilichofanywa leo sitakuwa katika kikosi cha Yanga niwatakie mafanikio yalio mema. Enjoy soccer.

Yanga kwa sasa inafanya maboresho ya kuimarisha kikosi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa msimu wa 2020/21.

Kwa msimu wa 2019/20 Ngassa alikuwa miongoni mwa wazawa ambao walikuwa wanatimiza majukumu yao na alitoa pasi ya mwisho kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Lipuli Uwanja wa Samora.

Mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni Julai 26 wakati wakisepa na pointi tatu zilizoipa nafasi Yanga kumaliza ikiwa nafasi ya pili na pointi 72.

4 COMMENTS:

  1. Na juu ya hao wakamtimuwa kavukavu. Inasikitisha alikuwa akiipenda sana Yanga

    ReplyDelete
  2. Hongera sana ni kati ya wachezaji waliopenda yanga kwa dhati

    ReplyDelete
  3. Huyu anaomba huruma ya mashabiki, ili wapige kelele uongozi umrudishe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic