August 31, 2020


 LEO Jumatatu saa 5:59 usiku dirisha la usajili litafungwa rasmi kwa hapa nchini ikihitimisha kipindi cha mwezi mzima cha timu kupewa kibali cha kusajili wachezaji wawatakao.

 

Baada ya kupita kwa kipindi hicho, ligi kuu rasmi sasa inaenda kuanza ambapo timu zote 18 zitakuwa na kibarua cha kugombea ubingwa ambao upo mikononi mwa Simba.

 

Tumeona Simba ambao jana walikuwa wanacheza mechi ya Ngao ya Jamii na Namungo, wametawala soka la Bongo kwa misimu mitatu mfululizo hii inaonyesha kuwa walijiandaa haswa.

 

Na msimu ujao pia utaona kama wamepania kuchukua taji la nne kama wapinzani wao wataendelea kuongea zaidi bila kupambana uwanjani.

 

Ninaamini kila timu imesajili kulingana na upungufu waliouona kupitia michuano mbalimbali ambayo walishiriki msimu uliopita.

Hivyo mpaka sasa maana yake kila kitu kiko sawa kwa ajili ya msimu ujao ambao ninaamini utakuwa na ushindani mkubwa haswa kwa kuwa timu zimetoka kujaza ‘mafuta’ hivyo tenki sasa limejaa.

 

Sasa msimu ujao tunataka kuona soka kweli na siyo malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza zaidi misimu iliyopita.

 

Najua malalamiko ya kwa waamuzi huwa hayakwepeki hata kama timu inaona ilizidiwa mchezo mzima lazima italalamika tu, cha kufanya punguzeni kuzungumza bali vitendo zaidi vinahitajika.

 

Tumeona wakati mnasajili mbwembwe zilikuwa nyingi kila timu ikitambia kuwa imenasa jembe, sasa hizo ndizo tunataka muzionyeshe ndani ya uwanja siyo tena maneno.

 

Unalalamika wakati mmefungwa bao moja na timu yako imeshindwa kufunga hata hilo moja, malizeni mechi uwanjani huku nje matokeo hayaweza kubadilishwa zaidi watafungiwa wahusika kwa makosa na msimamo unabaki kuwa vilevile.

 

Mwisho ni kwa wachezaji ambao wamesajili kwenye timu mpya. Najua huwa inachukua muda kwa baadhi ya wachezaji kuzoea mazingira mapya lakini ni vyema mkafanya kazi iliyowapeleka hapo mlipo.

 

Kuna wachezaji wamenunuliwa kwa fedha nyingi sasa mnapaswa kuhakikisha deni hilo mnalilipa kwa kucheza kwa viwango vya juu na kusaidia timu kufikia malengo yao.

 

Wapo wachezaji ambao wanazitumikia timu za taifa, hapa nitazungumzia zaidi wale wa Taifa Stars. Wamekubali kujiunga na klabu mpya pia wanapaswa kulinda viwango vyao kwa ajili ya taifa lao.

 

Tunafahamu kucheza haswa Yanga na Simba ni presha kubwa hivyo mnatakiwa kutulia na kufanya kazi yenu kwa umakini epukeni starehe na kujiona kama mmefika, zitumieni kama njia ya kwenda nje hizo klabu naamini mtafanikiwa.

 

Pambaneni ili kuhakikisha namba zenu timu ya taifa zinaendelea kuwepo. Ninajua ni changamoto kubwa kwa timu hizo ukiharibu katika mechi mbili basi ni ngumu kukuamini tena kwa dakika 90 zinazofuata hii maana yake unaweza kupotea mazima hata timu ya taifa unaweza usiitwe tena.   

 

Hivyo basi jilindeni kwa mapambano ya kuhakikisha mnazisaidia timu zenu na kulinda vipaji kwa ajili ya timu zenu za taifa.

 

2 COMMENTS:

  1. Kumbukeni kuwa marefa, ratiba kubadilikabadilika,na makandokandi ya mwaka Jana pia yawe yameisha

    ReplyDelete
  2. Marefa wanatoa Magoli ya offside,Tena kuna issue Morisson alipo kuwa Yanga Penalt hatupewi lkn upande wa pili mpaka Magazeti yameandika na juzi tumeona .Hapa Ni mpira Karia maelekezo .Halafu mkipigana vikumbo was mikia akazidiwa Hiyo fault,lkn akikuzidi nguvu huna stamina.Simba wamejiandaa hv virefa vyote vyao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic