August 26, 2020

 


KIUNGO mpya wa Yanga, Carlos Stenio Fernandez Guimaraes 'Carlinhos' baada ya kutua jana rasmi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,(JNIA) na kumalizana na mabosi wa Yanga, leo Agosti 26 ameanza mazoezi na wachezaji wenzake.


Yanga ilianza mazoezi Agosti 10, Uwanja wa Chuo cha Sheria ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6.

Mchezo wa kwanza kwa Yanga itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, Septemba 6.


Akiwa mazoezini ameonekana akiwa ni mwenye furaha huku akikaribishwa na wachezaji wenzake ambao tayari walishaanza mazoezi kwa kuimba naye na kucheza ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko.

Kiungo huyo aliyepokelewa na mamia ya mashabiki wa Yanga jana, Agosti 25 alipokuwa akitokea nchini Angola majira ya saa 7:20 amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya Yanga na anaahidi kufanya kazi zaidi kwa vitendo.

5 COMMENTS:

  1. Ingekuwa muonekano ndio kucheza mpira, huyu jamaa naona kama vile laini laini mno. Ila tusubiri shughuli yake uwanjani

    ReplyDelete
  2. Hivi wewe unajua ukomavu ligi nzima ya Tanzania Wachezaji wote laini Wengine misuli ya utapiamlo hawako physical Kama unavyo dhania mwache Kijana wa watu utashangaa mwenye hawa no jamaa ya hakina Kaka,de bruyne etc

    ReplyDelete
  3. Yelkpe vipi msuli wake au striker wa Simba Mbrazili,bila kusai papa Molinga kila akiguswa chini,shuti hata ukila K can't unadaka halafu brother Salehe anampamba hili Yanga tuingie Chaka tena

    ReplyDelete
  4. Msiwarudishe Yondani na Juma Abdul. Walikuwa ndio chanzo cha migogoro na migomo.Yondani alikuwa anagomea mechi mbalimbali tena muhimu.Timu kwa sasa ni nzuri na haina mamluki hata mmoja. Msiwarudishe heo watakuja kupandikiza chuki.

    ReplyDelete
  5. Majina mengi acha tuone uwanjani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic