August 5, 2020


MABADILIKO ndani ya kikosi cha Yanga kuelekea msimu wa 2020/21 kwa sasa yanaendelea baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

Miongoni mwa nyota 7 ambao waeachwa jumla ni pamoja na David Molinga ambaye ni mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga.

 Amecheza jumla ya mechi 32 ndani kati ya 38 za msimu huu akiwa  ametupia mabao 11 na pasi moja ya moja ya bao yeye ameachwa jumla kwa kuwa mkataba wake umekwisha.

Juma Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga msimu huu wa 2019/20 amekuwa bora ndani ya kikosi hicho.

  Ameanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 28 na ana jumla ya pasi sita za mabao zote amezimwaga kwa kutumia guu lake la kulia.

Yanga na Abdul kwa sasa wapo kwenye mazungumzo kuongeza dili jipya kwa kuwa  mkataba wake umemalizika.

Kelvin Yondani ameanza kikosi cha kwanza jumla ya mechi 22, mkataba wake umemeguka wapo kwenye mazungumzo kuongeza mkataba mpya ila bado mambo hayajawa sawa mpaka sasa wanavutana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic