RATIBA ya Ligi
Kuu England maarufu Premier League kwa msimu wa 2020/21, imetolewa leo Alhamisi
ambapo mechi zitaanza kuchezwa Septemba 12, mwaka huu.
Ratiba hiyo
inaonesha kwamba, siku ya ufunguzi zitachezwa mechi sita, kisha Septemba 14,
zitachezwa mechi mbili.
Mabingwa watetezi
wa Premier, Liverpool, wataanza kampeni ya kulitetea taji lao wakiwa nyumbani
Anfield kupambana na timu iliyopanda daraja, Leeds United.
Wageni wengine wa ligi hiyo, Fulham watakuwa nyumbani kupambana na Arsenal. West Brom ni dhidi ya Leicester City.
Wakati wengine
wakicheza wiki ya kwanza, mechi mbili ambazo ni Manchester City vs Aston Villa na
Burnley v Manchester United zimesogezwa mbele kutokana na Man United na Man
City kupewa muda zaidi wa kupumzika baada ya timu hizi hivi karibuni kutoka
kwenye michuano ya Ulaya.
Manchester United
na Manchester City, wenyewe wataanza kampeni zao Septemba 19, mwaka huu.
RATIBA
KAMILI KWA WIKI YA KWANZA IPO HIVI;
SEPTEMBA 12
Crystal
Palace vs Southampton
Fulham vs Arsenal
Liverpool vs Leeds United
Tottenham vs Everton
West Brom vs Leicester
City
West Ham vs Newcastle
SEPTEMBA 14
Brighton vs Chelsea
Sheffield vs Wolves
0 COMMENTS:
Post a Comment