UONGOZI wa Simba umesema kuwa kiungo wao Luis Miqussone,'Konde Boy' bado hajarejea Bongo kwa kuwa aliomba ruhusa ili aende akatimize jambo la msingi la kuoa.
Miqussone amekuwa akitajwa kuibukia kwa watani zao Simba ambao ni Yanga jambo ambalo limewafanya mabosi hao wa Msimbazi kushusha presha kwa mashabiki zao.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa baada ya Ligi Kuu Bara kuisha na kumaliza kazi kwa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho, Luis aliomba ruhusa akaoe.
"Niseme tu kwamba Luis aliomba ruhusa aende nyumbani akaoe hivyo bado ni mchezaji wa Simba na hakuna klabu ndani ya Afrika Mashariki ambayo inaweza kupata saini ya mchezaji kutoka Simba ambaye tuna mpango naye.
"Baada ya kuifunga Yanga mchezo wa Kombe la Shirikisho tulipokea ofa kutoka timu moja Netherlands, iliweka ofa kubwa ila tuligoma na kuwaambia kwamba waongeze dau," amesema.
Mwamba yupo zake Msumbiji kwa sasa amekuwa bora ndani ya msimu wake wa kwanza akitupia jumla ya mabao matano na pasi mbili za mabao kwenye mashindano yote ikiwa ni Kombe la Shirikisho akitupia mabao mawili na pasi moja ya bao na Ligi Kuu Bara ametupia mabao matatu na pasi moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment