August 5, 2020


JUMA Abdul, leo Agosti 5 ameachana na timu yake ya Yanga baada ya kushindwa kufikia makubaliano kwenye suala la mkataba wake.

Abdul ndani ya Yanga alikuwa ni nahodha msaidizi na kwa msimu wa 2019/20 amehusika kwenye jumla ya  mabao 6 kati ya 45 yaliyofungwa na Yanga akiwa ametoa pasi sita zilizoleta mabao.

Abdul amesema kuwa wameshindwa kuelewana na mabosi zake wa Yanga hasa kwa upande wa makubaliano ya mkataba wake.

"Tumeshindwa kufikiana makubaliano na Yanga kwenye upande wa mkataba wangu kwa kuwa walitaka kunipa mkataba bila ya kunilipa fedha za usajili hivyo nimeamua kuanza maisha mengine," amesema.

Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 ndani ya LigiKuuBara, Abdul alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi 28.

10 COMMENTS:

  1. Huu uongozi ujitafakari sana unawezaje kuacha juma?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao ndio walikuwa wanaivuruga timu kwa kuanzisha migomo isiyokwisha.Bado Yondani. Naye wamuache ili timu iondoe magugu yote.

      Delete
  2. Enter your comment...uyo aende bwana kama kaachwa ngasa yeye nan?

    ReplyDelete
  3. Safi sana , Yanga ni kubwa kuliko mchezaji na kama ameachwa ngasa iwe we Juma Abdul!

    ReplyDelete
  4. Huyu anaharibu timu ila ila Morison nidhamu yake ni nzuri aliyewaita manyani hakukosea

    ReplyDelete
  5. yaani kweli tunafata mikumbo ukweli, morrison yupo vizur ila kwa Juma ni mgogoro? et e

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic