CLATOUS Chama mwamba wa Lusaka, amerejea nchini tayari kwa ajili ya mchezo wa Simba day dhidi ya Vital'O ya Burundi, utakaopigwa Agosti 22 Uwanja wa Mkapa.
Chama alikuwa zake nchini Zambia kwa ajili mapumziko mafupi baada ya kumaliza kazi ya kwanza kwa msimu wa 2019/20 ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara na kutwaa taji la Kombe la Shirikisho.
Pia Chama alikuwa kwenye kikosi kilichotwaa taji la ngao ya Jamii hivyo amenyanyua jumla ya mataji matatu kwa msimu wa 2019/20.
Nyota huyo ana tuzo tano kibindoni alizotwaa msimu uliopita ikiwa ni pamoja na tuzo ya mchezaji bora iliyotolewa na Sport Pesa ambao ni wadhamini wakuu wa Klabu ya Simba, tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho, tuzo ya kiungo bora na mchezaji bora ndani ya ligi kuu pamoja na tuzo ya mchezaji ndani ya kikosi bora cha msimu.
Mchango wake kwenye ligi ni mabao mawili na kwenye kombe la Shiikisho ni mabao matatu.
Mabao ya kutengeneza kwenye ligi ni mabao 10 na kwenye Kombe la Shirikisho ni mabao manne.
0 COMMENTS:
Post a Comment