IMEELEZWA kuwa sababu zilizomwondoa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Senzo Mazingisa, ambaye Agosti 9 alitangaza kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu hiyo na ikielezwa kuwa amejiunga na Yanga SC ni kushindwana na waajiri wake wa zamani ambao ni Simba.
Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Championi na mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally Jembe, akizungumza katika kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio amesema kuwa moja ya sababu kuu zilizomwondoa Senzo katika Klabu ya Simba ni kwamba alishindwana na Simba kuhusu malipo ya mkataba wake mpya, kwani kiasi alichoomba kuongezewa, Simba waligoma kutoa.
"Kwanza ni kuwapongeza Yanga SC, lakini Simba SC wamepaniki sana, wanahisi Senzo ataondoka na Chama au Simba itayumba kimafanikio, Senzo ameikuta tayari Simba ina mafanikio, imekwenda Robo Fainali (CAF Champions League), ilikuwa imebeba ubingwa (VPL) mara mbili, Senzo hakuwepo.
“Yanga SC wana haki ya kufurahi sana kwa sababu walikereka Morrison kwenda Simba SC, na ninasikia walikuwa na sherehe ya kujipongeza, lakini Yanga wanapaswa kujua kwamba Senzo siyo kocha wala mchezaji, hawezi kuleta mafanikio ndani ya muda mfupi, wampe muda.
“Simba SC wanasema kazi aliyokuwa anaifanya Senzo alikuwa ameshawatoa sehemu ambayo kuna vitu hawakuwa wanavijua, baada ya hapo hakuna mwendelezo wa vitu vipya vyote wanavijua lakini walikuwa tayari kuendelea kufanya naye kazi, inawezekana hii ndiyo sababu inayowauma.
“Senzo atasaidia vitu vingi sana Yanga kuiboresha timu. Leo nilikuwa nahesabu, sasa ni mwaka wa 21 kila inapofika wakati wa usajili Simba na Yanga inakuwa burudani na hii ndiyo raha kwetu sisi watu wa michezo. Ni lazima mmoja amuumize mwingine sijui kwa nini?
“Mo na Senzo walikwaruzana kidogo, Mo alikuwa anataka Senzo aonyeshe progress (mandeleo) ya kwamba Simba ifanye nini baada ya muda fulani, iingize shilingi ngapi, tatizo timu zetu hapa nchini hazina target (malengo) kuhusu mapato.
“Niliandika makala kwenye Championi, najiuliza usajili unaofanywa na Yanga, pesa anatoa GSM au Yanga? Kama ni GSM anatoa kama msaada au atalipwa na Yanga, kama atalipwa ni lini na kwa mfumo gani? GSM wana nia nzuri na Yanga lakini mambo hayaendi, Yanga wawe na plan (mpango wa kueleweka).
“Mwaka jana nilikuwa Anfield nikarekodi video, sikutegemea kama Liverpool wanaweza kuwa wanauza maji ya kunywa kwenye duka lao, nguo za watoto, kava za simu vitu kibao. Yanga wana jezi nzuri sana lakini hakuna scarf, jifikirie kama maji ya Yanga leo yanauzwa wangapi watanunua?
“Tatizo la klabu zetu nchini hawana pesa zao binafsi hata kama zipo ni za wakubwa, wadhamini. Yanga kulikuwa na Manji alipoondoka ishu ya mishahara ikaanza kuwasumbua, hata GSM yupo leo siku akiwa hayupo itakuwaje? Simba vilevile kuna Mo, siku akiondoka itakuwaje?” amesema Saleh Ally.
“Yanga SC kumpata Senzo ni faida, kutokana na walivyokuwa wanajiendesha walitakiwa kupata mtu kama huyu, lakini najiuliza watamuingizaje kwenye mfumo wao, sababu kwa katiba ya Yanga hawana CEO, labda wampe Senzo ukatibu mkuu ili aweze kufanya majukumu yake.
“Ukisema Senzo kachukuliwa Simba SC ni makosa, sababu yeye na Simba walikuwa wameshashindwana, alikuwa huru kuondoka, aliomba kwenye mkataba mpya aongezewe mzigo, Simba wakasema mzigo huu hatuwezi kulipa. akasema mimi nitaondoka, Yanga wakapata taarifa wakamuwahi.
“Niliongea na Engineer. Hersi nikamwambia katika move zote ulizofanya kuelekea msimu ujao hii ya Senzo ni sahihi zaidi, sababu atakuwa mshauri mzuri, ni mzoefu, ana nafasi ya kumwambia hapa tumepatia hapa tumekosea, tunahitaji kocha wa namna gani, forward wa namna gani."
Jambo la Kwanza afanikiwe kuitetea Yanga yetu kutokana na maamuzi ya TFF kumhalalisha Morrison mchezaji wa Simba na hiyo ndio test yake ya kwanza ikiwa atatufaa au mla hela tu. Kaondoka kwa watani kwakuwa hawakumpa kila anachokitaka Bila ya kutimiza kile watani walitegemea kukifanya
ReplyDeleteAtakuja mchezaji mwingne
DeleteNyie washabiki wa Yanga acheni kujitoa akili ni busara tu zilizotumika nyinyi kuwa salama lakini kesi ingekuwa inaendeshwa kwa uwazi kama Mhakama za kwaida nyinyi mlikuwa mnashushwa daraja, karatasi za mkataba zimechanwa, tarehe za kusaini mkataba zinapishana ninachokiona mnataka kujiaminisha kama nyie ni wasafi mshasau mlivyosainisha Yondani, Mbuyu Twitwe, Ramadhan Kessy sajili zote hizo ingekuwa Serikali hii zilikuwa na matatizo kama haya ila Simba waliamua kuyamaliza kiutuuzima
ReplyDeleteWewe unaelewa adhabu ya kumsahinisha mchezaji mwenye matatizo wakati swala lake bado halijatolewa maamuzi na chombo chenye dhamana ya kutoa maamuzi. Hii ni dharau na utovu wa nidhamu kwa chombo husika na familia ya michezo kwa ujumla!
DeleteJe weee unaelewa adhabu ya forgery? mkata a wa morrison na barua ya uongo kwenda Azam
DeleteSuala sio kumsainisha mtu ambaye suala lake lina matatizo, simba walimsainisha kwa kuwa hakuwa na mkataba na ndio maana TFF wametoa majibu hayo japo hawakunyoosha maelezo
DeleteGSM noma sana aiseee kwakweli yani maana mikia fc wanateseka sana na kutapatapa lakini ndo hivo tena SENZO harudi mkiani
ReplyDeleteKaratasi mlizofoji hifadhini zitatakiwa huko mnapojipeleka wenyewe. Kuchamba kwingi......
DeleteSenzo hata akienda Yanga haisaidii..Simba ilifanya vema zaidi mwaka uliopita kabla ya yeye..Morrisoni ataichezea Simba bali Senzo hataichezea
DeleteYani Manyani f.c wao ndo wanaumia Morrison kuja Simba ila wanalazimisha Simba ionekane wanaumia kwa Senzo kuja kwao kinaletwa chombo kungine zaidi ya hiyo takataka yenu Senzo kudadadeki eti simba wanaumia kwa senzo kwenda Yanga nyie mnatakiwa mpelekwe milembe angekuwa muhimu sana huyo Senzo si angebaki kwao South Africa huko si ndo kuna ela nyingi kuna Mamelodi, kuna Kaizer Chiefs kuna Orlando Pirats mbona hawajamchukua mamweu kweli nyinyi
DeleteAdhabu yake nini?Una kanuni zako mwenyewe. Mchezaji hakuwa na mkataba halali. Hivyo ana haki ya kusain timu anayotaka.Hiyo kupelekwa kwenye kamati ya maadili ni kiini macho tu.
ReplyDeleteHata huijilikani unaongea nn au uko upande gni! Mana huna mbele wala nyuma!!
ReplyDeleteSawa huku anakoenda atapata hela zaidi...hivi kwani hajui ni mara ngapi Yanga hulipa mishahara ya miezi miwili pale ikiona mechi ya Simba imekaribia..Sitashangaa na huko wakimuandalia mkataba ambao haujui na sehemu ya sagihi
ReplyDeleteTunadanganyana tu Senzo hajaenda Yanga. ni utapeli kama mkataba wa Morrisoni...Kama barua ya Yanga kwa Azam eti ni Sure Boy ameiandika..Hiyo timu haina uadilifu...Inasikitisha namna wameachana na Molinga, tshishimbi, Niyonzima na Abdul
yanga daima mbele nyuma mwiko na nina imani mkataba ni sahihi na jambo la tarehe ya kuchapishwa na tarehe ya kusaini kuwa tofauti ni jambo la kawaida na wala sio kosa na tuna imani na viongozi wetu kua saini ya morison ni sahihi kwa sababu polisi walishaihakiki na kujiridhisha. twendeni CAS na haki itapatikana huko japo morison hatuna shida nae tena bali ni lazima tuwape fundisho hawa simba
ReplyDeleteSALEH MATAKO WEWE
ReplyDeleteWengine humu kama kwamba wamezaliwa wakitukana wakiwa wachanga
ReplyDeleteWengine kana kwamba walizaliwa wakiwa wanatukana
ReplyDeleteSuala sio kumsainisha mtu ambaye suala lake lina matatizo, simba walimsainisha kwa kuwa hakuwa na mkataba na ndio maana TFF wametoa majibu hayo japo hawakunyoosha maelezo
ReplyDeleteUkisoma comment za watu zimejaa ushabiki kuliko uhalisia. Hilo ndio tatzo la TZ kila kitu kipo kishabiki hata hukumu za mambo mengi zinasukumwa na ushabiki kuliko sheria. Simba na yanga zinafanya mambo yao kukomoana sio kimpira unavyotaka usajili haufanywi kulingana na mahitaji ya timu bali unafanywa kukomoana. Mtu anaweza akasajili kuogopa kwamba akisajiliwa na mpinzani atamsumbua lakin si kwa sababu anamhitaji kiufundi. Kuna timu naiona inasajili kwa fujo hapa
ReplyDelete