Imekuwa ikiripotiwa kuwa Yanga wapo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiungo huyo mzawa huku taarifa zikieleza kuwa tayari wameshapeleka ofa ili kuipata saini ya kiungo huyo.
Kwa kauli hiyo bado kupatikana kwa saini ya Sureboy Jangwani inakuwa pasua kichwa kwa kuwa Azam FC inaonekana bado wanahitaji huduma ya kiungo huyo.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa waliwahi kumuuliza Sureboy awali hakuwa tayari kuondoka kwa kile alichoeleza kuwa anafurahia maisha ndani ya kikosi.
"Tuliwahi kumuuliza mchezaji kama anaweza kuondoka ndani ya Azam FC alisema kuwa anafurahia maisha ya hapa na kwetu ni mchezaji muhimu ambaye tunamhitaji.
"Ili mchezaji aondoke ni lazima mambo yote yaende kwa usawa ikiwa ni pamoja na mchezaji mwenyewe anataka nini je na timu inahitaji kumuuza? Hakuna ambaye amesema mchezaji yupo sokoni kwa sasa.
"Hivyo ikiwa yeye atahitaji kuondoka hilo ni jambo jingine na uongozi ukiwa unamhitaji zaidi nalo ni jambo jingine ndio maisha ya soka yalivyo, hakuna ofa ambayo tumepokea kwa sasa zaidi ya kuskia tetesi lakini Sureboy ni Icon wa Azam FC," amesema.
Chezeeni wale wanaoitokea Roho hela ukiwaonesha 60,000 wanazitolea mate na sio Azam
ReplyDeletePole mbona Kama unataka kulia?hii ndiyo Yanga.pole mwandishi pole Simba fc
DeleteUNAJIFARIJI TU, ATASAINI TU YANGA.
ReplyDeleteManyani mpira ungekuwa unachezwa mdomoni kila mwaka mngekuwa mabingwa
DeleteYanga wanatengeneza timu mpya, hadi msimu ujao utaisha wachezaji wa yanga watakuwa hawajajuana hata majina...kaaaazi kweli kweli
ReplyDeletePorojo tu sasa hivi kuna watu wanaingilia move zote za Yanga kwenye Usajili....unajua kwanini kutangazatangaza na kutokuwa wasiri kwa mipango ya usajili watu wanapandisha dau kwa makusudi ama wanapewa mikataba wanaenda upande wapili wanauonyesha na mambo mengi ambayo yanafanya kukwama kwa tetesi zote....tatizo linaanzia Yanga na linaishia Yanga na haswa kwenye kuhusu Usajili wa wachezaji unaoendelea hivi sasa....Fedha ni kikwazo cha kwanza kikubwa hatima yake inaonekana na kutasfiriwa kwa. porojo zinazoendelea sasa hivi na maneno matupu njoo kesho nyingi!...mwishowe unaishia kwenye wachezaji kama Ninja...kwa undugu na kujuana!....kipa katoka (hamna kitu). Janja janja nyingi sana...maneno matamu sijui weka bando....sijui jiandae wiki ya mwananchi sijui mwakani ubingwa wetu, sijui tunajenga kikosi bora na cha ushindani.....maneno mengi ukija kwenye vitendo ndio hawa akina Ninja, yassin, mauya....nk. Tatizo ni pesa tusidanganyane hamna kitu.....matumaini "hewa" na matarajio ya uongo....msimu ujao maumivu yanaendelea....
ReplyDeleteHahaha haaaaa
Delete