August 30, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison ni mali yao na wamemtambulisha kuwa mchezaji wao wa 28.

Leo Agosti 30, Uwanja wa Mkapa ni siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo wanatambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2019/20 na timu hiyo.


Wakati wa utambulisho wa wachezaji hao ambao wametambulishwa na Mtangazaji na Mwadishi wa Wasafi Media ambae pia ni mchambuzi ndani ya Gazeti la Championi, Maulid Kitenge amesema kuwa bado Morrison ni mchezaji wa Yanga.


Katika utambulisho huo Kitenge amesema:"Mchezaji wa 28 ndani ya Yanga ni Bernard Morrison ambaye ni mchezaji wetu kwa kuwa kesi ipo CAS hivyo ni mchezaji wa Yanga."


Sakata la Morrison lilidumu ndani ya Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa muda wa siku tatu na baadaye maamuzi yalitolewa kuwa Morrison ni mchezaji huru hivyo anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote anayohitaji.


Agosti 8, alisaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba na amecheza mechi siku ya Kilele cha Simba day Agosti 22 wakati Simba ikicheza na Vital'O ya Burundi na ilishinda mabao 6-0 huku yeye akifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.


Leo pia Agosti 30 amecheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC wakati Simba ikishinda mabao 2-0, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 

11 COMMENTS:

  1. Hawa si bure ni heri wapimee kama wapo sawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga watakuwa wamependelewa kusajili wachezaji 11 wa kigeni kama Bernad Morrison bado ni mchezaji wao

      Delete
  2. Nukuu Kikwwte leo siku ya mwananchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Rais Mstaafu amewapa ushauri wa busara japokuwa uongozi wa yanga wameshapeleka shauri lao CAS

      Delete
  3. Hawapo sawa ndio mana wanaitwa kandambili aka vyura aka GONGOWAZI

    ReplyDelete
  4. Nna wasiwasi na mwandishi huyu

    ReplyDelete
  5. Kweli hii Ni utopolo, wanamambo ya kizamanizamaniii.Simba tunatwaa makombe wao wanawaza kujaza uwanja. Leo tayari kombe la kwanza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi kweli ni Yanga lakini viingilio vya chini vikilinganishwa na vya Simba day ndivyo vilivyojaza uwanja. Pia mashabiki wengine wameingia bure kwa kusukuma geti na kuwazidi nguvu walinzi

      Delete
  6. Utopolo wanadanganywa na wataendelea kudanganywa na viongozi wao na GSM, kwakuwa mashabiki,viongozi ni mambumbu kiufahamu. Mashabiki mshaliwa na GSM kwa morrisoni diyo wenu Tena mfuteni kwenye mawazo yenu

    ReplyDelete
  7. Morrison ni kama Jogoo na Jogoo kama hukulitunza na ukalifanyia fujo litahamia kwa jirani

    ReplyDelete
  8. Ni haki yao maana wasiposema hivyo kesi hewa itakuwa imefungwa. Ila wanajifurahisha tuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic