August 30, 2020

 


KLABU ya simba, leo Agosti 30 imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo FC na kufanikiwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Mabao ya Simba yalifungwa na nahodha wa timu hiyo, John Bocco kwa mkwaju wa penalti dakika ya saba baada ya Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 59 ambapo Morrison alipachika bao la pili kipindi cha pili ndani ya 18 kwa pasi ya Clatous Chama.

Ushindi huo unaifanya Simba kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kushinda mbele ya Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery.

Nyota wapya wa Simba, Joash Onyango, Larry Bwalya walifanya kazi kubwa kupambana kwa kuonyesha uwezo wao ndani ya uwanja.

Mchezo wa leo ni kifungua pazia kwa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6. Namungo ilipambana kwa kasi kipindi cha kwanza ambapo ilikuwa ikiwatumia nyota wao ikiwa ni pamoja na Sixtus Sabilo, Stephen Sey na Abdluhum Humud,

3 COMMENTS:

  1. Tushaanza kukusanya makombe ya 2020/21

    ReplyDelete
  2. na bado...miaka kumi back to back...kuanzia mwakani

    ReplyDelete
  3. Mbona watakoma GONGOWAZI safari hii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic