August 26, 2020

 


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amesema wapinzani wao Yanga na Azam nao wamefanya usajili mzuri, hivyo kutakuwa na ushindani mkubwa msimu ujao lakini akasisitiza watapambana nao na wasahau kuchukua ubingwa kwani wamepanga kuutetea.

 

Mo ameongeza kuwa nje ya kushindana na kutwaa ubingwa wa ligi lakini pia jicho lao ni kupambana katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Wapinzani wa Simba, Yanga wao hadi sasa wameshasajili zaidi ya wachezaji nane ikiwa ni pamoja na, Mghana Michael Sarpong, Mcongo Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Mcongo Mukoko Tonombe na Bakari Mwamnyeto.

 

Kwa upande wa Azam FC, wao wamezipata saini za Awesu Awesu, Mnyarwanda Ally Niyonzima, Mzimbabwe Prince Dube, Ismail Azizi na Danny Lyanga.

 

Mo amesema kuwa licha ya usajili huo wa wapinzani wao walioufanya kuwa mzuri, lakini wasifikirie juu ya ubingwa kutokana na kwamba wao wanalitaka kombe hilo.

 

“Tunataka kushindana kwenye ligi na tunajua wenzetu wamesajili vizuri na tuko tayari kushindana nao.

 

“Lakini malengo yetu ni kushinda ligi kwa mara nyingine tena na kupambana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, tunataka kufika mbali safari hii, tofauti na ilivyokuwa kwa msimu uliopita,” alimaliza Mo.

5 COMMENTS:

  1. Simba haitaki kuwavunja moyo watani ili watapocheza nao wacheze na morali kamili Bila ya visingizio

    ReplyDelete
  2. Kwahiyo anataka kutuaminisha kuwa Simba ndo regulator wa Team wapendwa Yanga na Team kama nne hv wamejipanga , Mimi Mr Salehe marefa hawa Wana mahaba Kama yenu najua watavuruga najua kwa huu usajili laZima tu

    ReplyDelete
  3. Masikini wao peke yao ndio daima wanaona wanaonewa na kudhulumiwa ambalo Hakuna timu yoyote nyengine yenye malalamiko yasiyokwisha na hilo ndilo linalowaumiza

    ReplyDelete
  4. Yanga wanasema wanamuuza mchezaji wa Simba Morrison kwa milioni Mia sita. Hivyo si vichekesho?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic