August 4, 2020


FARID Mussa, mchezaji huru mzawa mwenye miaka 24 inatajwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ili atue ndani ya kikosi hicho.

Mussa mzaliwa wa Morogoro, ndani ya uwanja nafasi yake ni kiungo mshambuliaji kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na CD Tenerife ya Hispania kufika tamati.

Mkataba wake uliisha Julai mwaka huu na hakupewa dili jipya la kusaini hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.

Ana uzoefu na Ligi Kuu Bara kwa kuwa aliwahi kuitumikia Klabu ya Azam FC kabla ya kuibukia ndani ya CD Tenerife, Aprili 2016. 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa uongozi kwa sasa unaboresha kikosi ambacho kitaleta ushindani msimu ujao wa 2020/21 huku akigoma kuwataja wachezaji walio kwenye mazungumzo nao.

"Tupo kwenye mchakato wa kufanya usajili baada ya kuachana na wachezaji wetu wengine ndani ya timu, kuhusu kuwataja wachezaji watakaokuja kwa sasa siwezi kusema ila tutawatambulisha utaratibu ukikamilika," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Faridi anafanya mazungumzo na Yanga hii Utopolo au Youngboys ya Switzerland?

    ReplyDelete
  2. Duh! toka Hispanics mpaka Tanzania kweli hii nihatari, Hamna kitu hapo unatoka juu inakwenda chini Kama kaburi Ni noma yaani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic