September 24, 2020


OFISA Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa Azam FC Uongozi wa timu hiyo ulishatia timu kitambo makao makuu ya Al Ahly na Zamalek kwa ajili ya kujifunza huku ziara nyingine ya kwenda Real Madrid ikikwama kutokana na janga la Corona.

Thabit amesema:" Januari mwaka huu, 2020. Mtendaji Mkuu wa Azam FC, (CEO), Abdulkarim Amin alienda jijini Cairo Misri kufanya ziara kwenye vilabu vya Al Ahly na Zamalek.


"Hivi ndivyo vilabu viwili vikubwa zaidi barani Afrika na mwaka 2000, Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, lilivitangaza kwamba ni vilabu bora vya karne ya 20.

"Katika ziara yake, Popat alijifunza mambo mengi juu ya namna ya kuendesha utawala na biashara ya soka, kuiweka klabu karibu na mashabiki pamoja kuboresha idara ya habari kama kioo cha klabu na chanzo cha mapato.

"Al Ahly ni klabu yenye idara kubwa sana ya habari ambayo inamiliki chaneli yake ya luninga inayoitwa Al Ahly TV ambayo huonesha mechi za kirafiki za klabu hiyo, mechi za vijana na mechi za michezo mingine kwa sababu klabu yao ya Sports Club, wana michezo mingi hai.

"Aliporudi nyumbani ndipo akaanzisha idara ya habari ya klabu.Mwaka huu alitakiwa aende klabuni Real Madrid kujifunza mambo mengine mengi kuhusu soka ili kuleta ufanisi kwenye klabu yetu.

"Lakini bahati mbaya ndiyo ukazuka ugonjwa wa Corona uliosimamisha mambo mengi duniani.
Lakini Inshallah, mwakani inawezekana ziara hii ikafanikiwa.

"Hata hivyo, baadaye mwaka huu ataenda Afrika Kusini kwenye vilabu vya Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates katika muendelezo wa ziara za kujifunza namna bora ya kukuza klabu."

11 COMMENTS:

  1. Hayo ndio tunataka ili soka letu lisonge mbele. Sio kutegemea kamati za ufundi toka gamboshi

    ReplyDelete
  2. Hawa simba sasa kidgo wanataka kuiga, Mara wanataka uwanja, ekedemy,kwenda kwa al ahly wakati wenziwao washayafanya kitambo

    ReplyDelete
  3. Kujenga uwanja , Academy na kwenda kutembelea Al Ahly ni kuiga kweli kazi ipo? MANYANI FC

    ReplyDelete
  4. Baadhi ya utopolo bdo wajinga kifikra Kama huyo hapo juu 👆. Hajui ukitaka maendeleo tembea/Jenga urafiki na aliyeendelea na iga kwa lengo la kupiga hatua mbele. Upungufu wa fikra baadhi wanawaza kwenda chini au kubaki hpo alipo. Criticise for development only. Huna point kalale

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic