September 5, 2020


 

UONGOZI wa Simba umesema kuwa Mtendaji Mkuu mpya ndani ya Simba  (CEO), atakuwa ni  Barbara Gonzalez ambaye atarithi kiti cha Senzo Mbatha.


Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa ni makubaliano ya uongozi jana ambapo walikuwa na kikao cha Bodi ya Wakurugenzi, Septemba 4.


Anakuwa CEO wa kwanza wa kike ndani ya Bongo kwa msimu wa 2020/21 kuiongoza klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi. 


Mbatha yupo ndani ya kikosi cha Yanga ambapo aliibukia huko muda mfupi baada ya kujiuzulu ndani ya Simba.

29 COMMENTS:

  1. Simba bwana inatupa raha mrembo sasa CEO tumeletewa

    ReplyDelete
  2. Hii ni surprises kubwa kuliko helicopter

    ReplyDelete
  3. Asante Mo walau umetupoza. Historia ya Simba ya watu ma handsome ma beautiful. Kutuletea sisi wa Sudan kusini! Mababu!

    ReplyDelete
  4. Wanawake Mara nyingi wanakuwa na misimamo hasa wasomi asante Mo na kamati yako kutuletea iron lady kwenye football

    ReplyDelete
  5. Mweee Thoooo ,tujifunze level ya Senzo na huyu dada na Thimba mmekamatwa.mikia

    ReplyDelete
  6. Simba usawa ndo jadi yetu na tunaiendeleza

    ReplyDelete
  7. Simba ombeni usiku na mchana mchukue ubingwa, mkiukosa ndio mtajua kwamba MO ni mwekezaji au mfadhili!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kuchukua ubingwa ni kila timu inatakiwa kufanya hivyo siyo Simba tu.... huyo Senzo mkikosa ubingwa hakuna amani hapo

      Delete
  8. Huyo dada amejaa madini ya utajiri katika utendaji senzo cha mtoto.Simba ilihitaji CEO mbunifu sio uzoefu tu pekee yake. Dada msomi zaidi kwenye masuala ya makuzi ya mtaji na simba inahitaji kukua kiuchumi ili iweze kujiendesha kwa faida ni kazi ya kitaalam zaidi na mtaalam ndie huyu Dada hongera simba kwa kuacha siasa na kuona mbali zaidi na Yanga nao waige ya hii ya CEO mdada inalipa.

    ReplyDelete
  9. Kinachotusumbua wabongo siyo Elimu au usomi bali kubadilisha usomi wetu au Elimu tulizonazo kwenye vitendo yaani utendaji wa faidi ya wengi

    ReplyDelete
  10. Yanga igeni mnyama,mahesabu 1,2.. ya tatu muda cmrefu senzo anatimka/ mnamtinua Utopolo

    ReplyDelete
  11. Profile yake msiwe na shida nayo yupo vzr ila wale wachezaji wahuni wawe makini kwa huyo namfahamu nishasoma na mdogo wake hivyo sifa zao Ni kabambe

    ReplyDelete
    Replies
    1. *SIMBA AMKENI*

      *Barbra anakamilisha mpango wa kuiteka Simba*

      Mohammed Dewj amekuwa na mpango (mission) ya kuiteka Simba kwa Miaka mingi, mpango wake sasa unakamilika rasmi baada ya kumteua Barbra shwahiba wake na msiri wake mkubwa katika mipango yake michafu.
      Mpango wa MO kuiteka Simba ulikuwa unafeli mara zote kwa kuwa Simba ilikuwa na viongozi makini, hivyo kupata matatizo kwa viongozi wa Simba, Evans Aveva na Nyange Kaburu kulimpa nafasi MO kuwatumia viongozi dhaifu na wenye tamaa kama Salim Try Again kufanikisha jambo lake.

      *Mpango ulianza hivi*

      MO alimuahidi fungu nono Try Again aliyekuwa anakaimu Urais wa Simba SC, hivyo Try Again akashirikiana na Barbra kuandaa mpango butu wa Uwekezaji huku wakiutumia Mdomo wa Haji Manara.

      Try Again alihusika kukwepa ushauri wa Kamati ya Jaji Mihayo na kuwapumbaza Wanasimba kwa Pilau na Biriani pale JNCC hatimaye wakakubali mabadiliko hewa ambayo sasa ni Mwaka wa tatu hayatekelezeki.

      Baada ya kazi kubwa ya kuuza Simba kwa MO, Try Again hakutaka kuombea uongozi Simba SC, walimpanga mtu wako ambaye alishindwa na Swedi Nkwabi, hivyo kazi ikawa kubwa tena maana Swedi alikuwa anahoji sana.

      Hivyo Basi wakaanza kumpiga vita Swedi na hatimaye akaondoka hivyo Simba ya Wanachama ikabaki na wajumbe dhaifu akina Kaduguda na Asha Baraka watu ndio mzeee.

      Try Again akateuliwa na MO kama Mjumbe wa Upande wake na akampa Umakamu Mwenyekiti wa Bodi yaani Mwenyekiti anatoka Upande wa 49% na Makamu anatoka huko huko, wenye 51% tupa kule na hawana hela hiyo hawana cha kusema.

      *Sasa basi mpango wa MO kuiteka Simba uko hivi*

      MO alikwama kibiashara na Kampuni zake zilizokuwa na jina la MeTL zilizokuwa na maedni.mengi ya Kodi na kutoka Bank, alijuwa Simba ndio itamuinua, akabadili jina la Brand na kuziita MO, na hapo akaanza kuihuaisha MO na Simba akaanza na MO Foundation kwanza, kisha bidhaa Zote Ikawa MO nazo akazihusisha na Simba.

      Barbra akiwa Mtendaji Mkuu wa Foundation hiyo kwa Siri Siri aliandaa andiko na kuiunganisha taasisi hiyo na bidhaa zingine za MO na Klabu ya Simba na walifanikiwa bila hata kushirikisha Wanachana.

      Baada andiko kupitishwa, kwa Siri pia kila kitu cha Simba iliamuliwa na Bodi kiwekewe jina MO mbele yake.

      Hii ndio sababu ya MO Simba Foundation, MO Simba Awards (zote Tuzo), Logo ya Klabu na Kaulimbiu ya Kiswahili, ambapo MO ameweka Simba wake aliyemtumia wakati akianzisha African Lyon na ule Uwanja aliouita MO Arena ambao MO hajachangia chochote Japo anasema Katoa pesa (nitauelezea andiko lijalo).

      Baada ya haya yote, tayari Barbra na kina Try Again wameshaandaa andiko lingine ambalo limeshafika TFF na Rais Karia na Katibu wake Kidao wanajua na wanahusika ambapo MO na wenzake wanakusudia kubadili jina la timu kutoka Simba SC na kuwa MO Simba FC.

      Baada ya hapa, hakutakuwa na Simba SC tena kwenye Logo Kuu, hakutakuwa na Nguvu Moja, wanaojiita Wanachama wa Simba hawatakuwa na kauli yoyote na wakidai wataambiwa Simba SC haipo na kweli hata kwenye usajili wa Ligi haitakuwepo.

      Karia na Kidao hawana namna, wameshikwa pabaya, maana hatima yao Madarakani pia imeshikwa na Hawa jamaa wa MO Simba. Endeleeni kutega sikio CEO Barbara anakuja kufanya yake.

      Delete
    2. Mbona unatumia nguvu kubwa hivi kajambo kenyewe kadogo hivi?

      Delete
    3. Yani mtu akikwambia akili zako kama shabiki wa yanga pigana huyo aliyeandika hayo malezo marefu hapo juu hivi anafikiri simba inashabikiwa na watu mazumbukuku kama yeye tu, simba ni klabu inayoshabikiwa na watu wenye vyeo vikubwa nchi hii kama hujui, ETI MPANGO ULIANZA HIVI, yani kuna vijitu kwenye hii nchi vinajitafutiaga matatizo vyenyewe kikiitwa kiende kuthibitisha kilichoandika hapo juu kitaona kimeonewa,huyo MO hana uwezo hata chembe kwa taarifa yako wa kuiteka Simba we kama unaona hizi timu zipo zinacheza cheza tu viwanjani ukajua unaweza kwenda tu na kujimilikisha waongopee hao hao wasiojua mizizi ya hizi timu.

      Delete
    4. Eti MO hajachangia chochote kwenye ujenzi wa uwanja wa simba , sasa Simba walikuwa wanakwama wapi kwenye ujenzi wa huo uwanja na nyasi bandia zilikuwepo muda mrefu na zilikuwa zimezuiliwa bandarini, mbona Mo alipoichukua tu simba ujenzi ukaanza, au MO ndo alikuwa anazuia ujenzi wa huo uwanja muda mwingine chizi sio mpaka aokote makopo, eti nitaelezea andiko lijalo, ushasahau wale wajumbe wa Yanga waliojiuzuru kawaulize vizuri watakwambia GSM wanataka kufanya nini pale Yanga chizi wewe, muda utaongea

      Delete
  12. WAZIRI KIGWANGALLA ASHANGAA MO DEWJI KUMTEUA MSAIDIZI WAKE BINAFSI KUWA CEO SIMBA
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk HamisI Kigwangalla ametilia shaka uteuzi wa Msaidizi Binafasi wa Bilionea, Mohjamed ‘Mo’ Dewji, Barbara Gonzalez kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya Simba SC.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mo Dewji leo amemtangaza Barbara Gonzalez kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, akiziba nafasi ya Muafrika Kusini, Senzo Mazingisa Mbatha aliyehamia kwa watani, Yanga SC.
    Lakini saa chache baada ya uteuzi huo, Kigwangala akaandika kwenye ukurasa wake wa twitter; “Kuna ujanja na Kuna ujanja ujanja. Ujanja ni pale @SimbaSCTanzania tulipokubali kuhama kutoka kuwa Klabu ya Wanachama na kuwa Kampuni. Ujanja ujanja ni hiki kinachoendelea sasa hivi; hisa hazijalipiwa. PA wa mwekezaji ambaye hajalipia shares anateuliwa kuwa CEO,”.

    Kigwangalla ameongeza kwamba mabadiliko yaliyompa Mo Dewji Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC hayajakamilika kwa kuwa hajalipa Sh. Bilioni 20, lakini ajabu anafanya maamuzi anavyotaka.
    Mo Dewji akamjibu Kigwangalla katika mjadala uliovutia watu wengi wenye mawazo tofauti; “Mhe.Kigwangalla, sio utu kumuombea mtu yoyote apigwe mawe. Suala la uwekezaji Simba nililielezea kwenye interview na WasafiFM. Wengi wameelewa. Itafute. Kama bado hutaelewa, namba yangu unayo nipigie nitakufafanulia. Pia nisamehe kwamba mkopo wa pikipiki ulioniomba haikuwezekana,”.
    Hivi karibuni Mo Dewji alisema kwamba mfumo wa mabadiliko bado haujakamilika hivyo si wakati mwafaka kuzungumzia uwekezaji wake wa Sh. Bilioni 20 katika klabu hiyo. “Bilioni 20 zipo, kwa sasa kila mwaka natoa bilioni 3 kama ruzuku kwa klabu. Naamini asilimia kubwa ya Wanasimba wananielewa, kama hunielewi, basi,”alisema.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kigwangala ana mataizo ya kudhau wawanawake ni tabia ya hovyo.Halafu ilianza kagere kampiga kocha. Halafu ikaja hii Mkude kapigana na wawa. Sasa leo kuna nyengine hapa Mo anataka kuipora simba? Mo aipore simba aipeleke wapi? Upi wakati bora? simba kabla ya Mo au simba baada ya Mo kuamua kuekeza simba? Fursa za hisa bado zipo simba lakini sidhani kama kajitokeza meanwhile wa simba kununua angalau asilimia kumi 10 ndani ya 51 hisa za wanachama? Simba ya aveva na kaburu na simba ya Mo ipi bora? Hapana shaka kuna watu wanaumia kuiona simba ilivyo sasa.Hao watu wanao hoji simba ya Mo hawana tofauti na hao watu wanaohoji kwanini Magufuli kajenga fly over? Nchi hii ina wachawi wa maendeleo wengine huwezi kuwafikiria kuwa ni wanga.Wanachokitaka ni kuiona simba ikirudi nyuma na kuanza kutembeza bakuli..Mungu ampe Mo moyo wa subira ila sisi wabongo kwa majungu tunamzidi Iblisi.

      Delete
  13. JPM ameleta heshima kubwa sana kwa Nchi. Haya yote siku za nyuma hayakuwepo. Matajiri biashara za ujanja zimechina. Sasa hivi wanatafuta fedha kwenye Club zenye utajiri wa wanachama. WANACHAMA NA NYINYI HAMKENI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amkaa wewe...sie tunaendelea kulala na ndoto zetu za MO.Usitufokee...Pimbii wewe

      Delete
  14. Yani mtu anaandika maelezo marefu kana kwamba anajua kila kitu kinachoendelea Simba ukweli ni kwamba simba inawakera watu wengi sana (mashabiki wa utopolo fc)kwa hiyo jambo lolote likitokea simba wanataka kutumia nguvu nyingi kuwaaminisha watu kwamba pale simba kuna matatizo, ili simba wavurugane alafu ndipo wao wapate mafanikio mmechelewa kweli Rais Magufuli ameshabariki mabadiliko simba, na tunajua ili tufikie mafanikio kuna vishanta wengi tu ambao watakuwa wanaleta chokochoko lakini Simba ni nguvu moja, Nnachojua mimi Yanga ilianzishwa kwa ajili ya Siasa , Simba ilianzishwa kwa ajili ya mpira hasa na ndio mana mambo mengi ya kimaendeleo ya kimpira wameanza Simba alafu yanga ndo wanakuja wanaiga, Mo AMEKUWA TAJIRI KABLA HATA HAJAICHUKUA HIYO SIMBA, na wewe uliendika hapo juu kwamba Mo anataka kubadilisha jina la simba na kuwa Mo simba sports club, NAFIKIRI HATA YANGA MUDA SI MREFU ITAITWA GSM YANGA SPORTS CLUB

    ReplyDelete
    Replies
    1. Samahani hivi yule Mwenyekiti wa Simba aliyejiuzulu (Nkwabi) na Dr. Kigwa nao ni Yanga?

      Delete
    2. Kumbe ulikuwa hujui kuwa ni Yanga.Unauliza swali wakati jibu unalo.

      Delete
  15. kUMBE ROHOOOO ZINAWAUMA, KUMBE ROHOOO ZINAWACHOMAAA nakumbuka ule wimbo wa Mr. Blue, manyani fc wanateseka sana na simba, eti Mo ana mission ya kuiteka simba yani kwa akili yako ilivyokuwa fupi Serikali walivyoweka asilimia 51 kwa wanachama na 49 kwa mwekezaji ulifikiri wao hawana akili, andika malezo yako marefu wadanganye hao hao wasiojua nini maana ya SHARES, yani mtu ana asilimia chache anawezaje kujimilikisha timu , kweli nimeamini yale maneno ya LUC EYMAEL " AKILI ZENU NI KAMA WOO! WOO1 WOO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vipi CEO mpya ana baraka za wanachama?
      Ruksa povu

      Delete
    2. Baraka za wanachama zimebarikiwa na wawakilishi wao wakurugenzi ndani ya bodi.kama siko sahihi basi tuletee kipengele hicho kilichopo ktk katiba ya Simba ili nasi tujiridhishe.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic