COASTAL Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda leo Septemba 28 imesepa na pointi tatu kwa mara ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 bila kuambulia ushindi zaidi ya sare.
Bao pekee la ushindi kwa Coastal Union lilipachikwa dakika ya 87 baada ya mabeki wa JKT Tanzania kujichanganya kuokoa hatari ambapo Edson Katanga alijifunga dakika ya 87.
Mchezo wa kwanza Coastal Union ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Namungo kisha ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC na ililazimisha sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkwakwani.
Leo imeibukia mbele ya JKT Tanzania ambaowamewapa zawadi ya ushindi wa pointi tatu kwa mara ya kwanza. Safu ya ushambuliaji ya Coastal Union bado haijaambulia bao ndani ya dakika 360.
Ushindi huo unaifanya Coastal Union kufikisha jumla ya pointi 4 ikiwa nafasi ya 14 huku JKT Tanzania ikiwa nafasi ya 13 na pointi nne wakitofautiana kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungana.
Mchezo wa leo ulikuwa ni wa mwisho kukamilisha mzunguko wa nne ambao ulikuwa ni wa ushindani mkubwa na umeshuhudia bao moja la leo la kujifunga ndani ya dakika 90.
Nina wasiwasi mwendo wa Coastal mwaka huu utakuwa kama Aston Villa msimu uliopita,tusubiri tuone
ReplyDelete