September 29, 2020


 JANA Septemba 28, Ligi Kuu Bara mzunguko wa nne ulikamilika kwa mechi tisa kukamilisha kazi yao ya kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.


Kwenye mechi hizo tisa ambazo zilichezwa ni mechi moja waligawana pointi mojamoja ambapo ilikuwa ni kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Biashara United ilichezwa Uwanja wa Uhuru na dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana.


Mechi mbili zilikusanya mabao mengi zaidi ilikuwa ni ile ya Polisi Tanzania 3-0  Dodoma Jiji,  Uwanja wa Ushirika Moshi pamoja na ile ya Simba 3-0 Gwambina Uwanja wa Mkapa na kufanya jumla yapatikane mabao sita kwenye mechi hizi mbili.


Mchezaji aliyetupia mabao mengi ni Marcel Kaheza alifunga mabao mawili wakati Polisi Tanzania ikishinda mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji kisha supa sub ni Chris Mugalu alitupia bao moja kwenye ushindi wa mabao 3-0 kwa Simba mbele ya Gwambina alichukua nafasi ya Meddie Kagere.


Jumla yamefungwa mabao 13 kwa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kinara ni Azam FC ana pointi 12 huku David Kissu akiwa ni kipa mwenye clean sheet nyingi kuliko wote kwa makipa kibindoni anazo nne kwenye mechi nne alizodaka ndani ya Klabu ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic