September 28, 2020

 


MANCHESTER United imesema kuwa itatumia nguvu kubwa kumpata nyota wa Borrusia Dortmund, Jadon Sancho ambaye inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi hao.


Sarakasi za kuipata saini ya Sancho kuibukia Manchester United zimekuwa zikiripotiwa kukwama mara kwa mara ambapo United inaelezwa kuwa iligomea dau ambalo mabosi hao walitaja.


Dortmund inahitaji euro milioni 100 ili kumuachia nyota huyo kuibuka ndani ya Old Trafford.


Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar amesema kuwa kwa sasa ni ngumu kuweka wazi kuhusu masuala ya usajili ambapo mpango wa kusajili mabeki kwenye kichwa chake haupo.


"Bado kuna uhitaji sehemu kadhaa lakini kwa upande wa mabeki nina amini kwamba hawa waliopo watafanya vizuri," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Haya o.g.s na wafanye vzr lkn pia unatushangaza usajiri wenyewe sio mzuri wa kubahatisha Sana na kusua sua unatuumiza mashabiki wa man united

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic