September 13, 2020

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, jana walibanwa mbavu mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wao wa pili mzunguko wa pili kwa kufungana bao 1-1.

Simba walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 44 kupitia kwa kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mzamiru Yassin baada ya kiungo Baraka Majogoro kufanya makosa nje kidogo ya 18 ambapo baada ya kufunga bao hilo kiungo huyo mzawa aliwaomba msamaha mashabiki wa Mtibwa Sugar

 Bao hilo la Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck liliwekwa sawa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro dakika ya 46 kwa kichwa kilichofungwa na Boban Zingiratius katikati yam situ wa mabeki wa Simba akimalizia pasi ya Issa Rashid baada ya mlinda mlango Aishi Manula kuacha lango wazi.

Jitihada za Simba kusaka pointi tatu na Mtibwa Sugar kulipa kisasi cha mchezo wao wa mwisho msimu uliopita kwa kufungwa mabao 3-0 na Simba Uwanja wa Jamhuri ziligonga mwamba.

Mikono ya Abubakari Twalib, mlinda mlango wa Mtibwa Sugar iliweza kuokoa hatari za nyota wa Simba waliokuwa wakiongozwa na John Bocco ikiwa ni pamoja na ile iliyopigwa dakika ya 24 na Clatous Chama,dakika ya 31 kupitia kwa Bocco, dakika ya 34 kupitia kwa Jonas Mkude na Joash Onyango dakika ya 42 kichwa chake kiligonga mwamba,Luis Miqussone dakika ya 83.

Mikono ya Manula nayo ilikutana na balaa ambapo dakika 27, Juma Nyangi alipita katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kuachia shuti kali ambalo liliokolewa,Ibrahim Hamad Ibrahim naye alifanya jaribio kali dakika ya 29 ila alikosa na jaribio kali kwa Mtibwa Sugar lilifanywa dakika ya 85 na Jaffary Kibaya likaokolewa na Manula.

Mtibwa Sugar inalazimisha sare ya pili ikiwa nyumbani baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo na jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba.

4 COMMENTS:

  1. Acha upuuzi..Yanga ilipotoa sare hukutaka kuandika kuhusu matokeo hayo..actually hukuandika chochote baada ya mchezo huo..
    mchezo wa Simba tayari umeishaandika alichopost haji manara, eti Sven kasema kitakachoikosesha ubingwa Simba, na hii havari.,
    inaonekana timu ya Simba inaishi bure bila kulipa kodi kwenye ubongo wako.

    ReplyDelete
  2. mwandishi mshenzi huyu! Simba kutoa sare ndiyo imekuwa habari...Yanga kutoa sare mchezo ukawa umeisha..Kilichoandikwa ni Yanga yawashukuru mashabiki kujitokeza kwa wingi,,Simba kutoa sare habari inarudiwa rudiwa kama vile ile ya "yule muuaji wa simba" ..haifai

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😆😆😆 mwandishi anatuongezea munkari Simba tutwae ubingwa mapema bila yeye kujitambua

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic