September 13, 2020


 

MCHEZO wa ufunguzi wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool dhidi ya Leeds United uliochezwa Uwanja wa Anfield na mabingwa hao watetezi kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 unatajwa kuwa ni miongoni mwa mchezo bora wenye ushindani kutokea kwa kuwa ulikusanya mabao mengi ambayo ni saba.

Kwenye mchezo huo shujaa alikuwa ni nyota wa Liverpool, Mohamed Salah ambaye alifunga hat trick yake ya kwanza alianza kufunga bao la kwanza dakika ya nne kwa penalti na bao la pili alifunga dakika ya 33 huku lile la mwisho na la ushindi kwa timu yake alipachika dakika ya 88 kwa mkwaju wa penalti na bao moja lilipachikwa dakika ya 20 na beki Virgil Van Dijk dakika ya 20.


Mabao ya wapinzani wao Leeds United yalipachikwa dakika ya 12 kupitia kwa Jack Harrison dakika ya 12,Patrick Bamford dakika ya  30 na Mateusz Klich dakika ya 66.


Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa mchezo ulikuwa wenye ushindani na vijana wake wamepambana kutafuta ushindi huku wakikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao ambao nao pia walikuwa vizuri.


Timu zote mbili zilikuwa zinacheza kwa kushambulia huku zikiwa na hesabu kubwa za kupata ushindi mwanzo mwisho jambo ambalo liliongeza utamu wa mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic