BAO la faulo la kitasa wa Simba, Muivory Coast, Pascal Wawa, limemuibua kocha wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck kwa kusema kuwa alimisi kuona mabao ya aina hiyo kwenye timu hiyo.
Sven
ameongeza kuwa aina ya mabao hayo ya mipira ya adhabu kwa kiasi kikubwa
aliyamisi kuona yakifungwa ndani ya kikosi hicho kutokana na kupoteza nafasi
hizo mara nyingi wanapopata.
Wawa
alifunga bao lake la kwanza la msimu huu kwa faulo katika mechi dhidi ya
Gwambina FC, kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Septemba 26.
Sven amesema kuwa licha ya uzuri wa bao hilo pia Wawa ni
mfungaji mzuri wa mipira hiyo ambapo ameshawahi kufanya hivyo kwenye mechi zao
za msimu uliopita.
“Tulifunga
kwa njia ya mipira ya adhabu, hiki ni kitu kizuri kwa sababu kwa muda mrefu
hatukufunga, nafikiri hii ndiyo mara ya kwanza tumefunga kwa namna hiyo baada
ya muda mrefu sana.
“Wawa
(Pascal), anajua kupiga mipira hiyo ya adhabu, msimu uliopita kwenye mechi
dhidi ya Azam FC na Yanga alichukua jukumu hilo la kupiga na kufanya vizuri.
Lakini pia tuna wapigaji wazuri wa mipira hiyo akiwemo Miquissone (Luis)
aliyepiga lakini kipa alitoa,” alimaliza Sven.
Katika
mchezo huo, Simba walipata ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo mkali uliopigwa
kwenye Uwanja wa Mkapa.
Simba kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 10 sawa na Yanga iliyo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi nne huku vinara wakiwa ni Azam FC wenye pointi 12, Gwambina ipo nafasi ya 17 na pointi moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment