September 22, 2020

 




Mchezo wa kirafiki kati ya Simba na African Lyon uliochezwa leo Septemba 22 Uwanja wa Azam Complex umekamilika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mabao ya Simba  yalipachikwa kimiani na Chris Mugalu dakika ya 46 kwa pasi ya Ibrahim Ajibu na bao la pili lilipachikwa kimiani na Charlse Ilanfya dakika ya 53 kwa pasi ya Gadiel Michael.

Kwenye mchezo wa leo mashabiki walijitokeza wengi kipindi cha pili baada ya mpira kuanza kipindi cha kwanza ukiwa na mashabiki wachache kiasi chake.


Dakika 45 za kwanza timu zote zilitoshana nguvu na kuwafanya Simba pamoja African Lyon kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana ila mambo yote yalibadilika kipindi cha pili.

African Lyon ipo kwenye maandalizi ya kujiaandaa kwa ajili ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa ipo kundi A huku Simba ikijiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.

5 COMMENTS:

  1. Mazoezi tu, ubingwa lazima iwe iweje

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Kawa ulize walikuletea jezi za desing ya pampers

      Delete
  3. Mugalu mechi tatu goli tatu huyu sio straika wa kawaida. Kama atakuwa fiti na akatumika vizuri basi simba watatangaza ubingwa mapema zaidi kuliko msimu uliopita.

    ReplyDelete
  4. Yah! waambie hao utopolo nawengine, wasicheze na mnyama wataliwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic