ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar aesema kuwa mchezaji wake Boban Zirintusa kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga uliochezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati wakipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mpira ulimkataa jambo lilimfanya akamtoa mapema.
Zirintusa bado hajasaulika kwa mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula baada ya kumtungua bao moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 wakati Simba iipocheza nao Uwanja wa Jamhuri kwenye mchezo wa ligi.
Wakati timu yake ya Mtibwa ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga nyota huyo ambaye alitibua 'clean sheet' ya Manula alitumia dakika 36 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Nyangi.
Katwila amesema:"Unajua mpira ni mbinu sasa kwa namna ambavyo nilimuona Zirintusa kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga mbinu zangu kwake zilikwaa hasa kwenye mipira ya juu ambayo ilikuwa inapotea kwake.
"Nilimuona anapata tabu uwanjani, alikuwa anazungukazunguka kutafuta mipira huku ile ya juu akiwa anapishana nayo jambo ambalo lilinifanya nikamtoa mapema ili kwenda na kasi ya mpira.
"Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa ila mwisho wa siku matokeo tuliyopata tumpoteza tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo," amesema.
Mtibwa Sugar kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 9 kibindoni ina pointi 5 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na kibindoni ina pointi 10.
Timu zitaenda zinajipambanua zenyewe hatua kwa hatua ila top 3 watabaki Azam, Simba na Yanga na bingwa atatokana na timi hizo.
ReplyDeleteKamati ya utopolo hatar sana piga pin wasumbufu wote duu
ReplyDeleteHujielewi ww nyie mikia fc ndio wanga mpaka mashabiki
Delete