September 29, 2020

 


LUIS Miqussone, kiungo mshambuliaji wa Simba ameshindikana ndani ya Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kwa kuwa amehusika kwenye mabao manne kati ya 10 ambayo yamefungwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

 

Simba ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 10, imefunga jumla ya mabao 10, ambapo matatu ilifunga kwenye mechi zake za ugenini ilikuwa mbele ya Ihefu wakati ikishinda mabao 2-1 na bao la tatu lilipatikana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

 

Ilipotua kwa Mkapa ikiwa imecheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 imefunga jumla ya mabao saba huku kinara wa kutengeneza mipango ni Luis ambapo ametengeneza jumla ya pasi nne za mwisho zilizoleta mabao.

 

Alianza wakati Simba ikishinda mabao 4-0 mbele ya Biashara United kwa kupiga ‘hat trick’ ya pasi za mabao na yalijazwa kimiani na Clatous Chama aliyefunga mabao mawili pamoja na nyingine alimpa Meddie Kagere.

 

Wakati akitimiza dakika yake ya 270, akiwa na wastani wa kuwa hatari kila baada ya dakika 67 uwanjani kwa kuwa amecheza mechi tatu na zote ameyeyusha dakika 90,  mbele ya Gwambina, Simba ikishinda mabao 3-0, alitengeneza pasi moja ya bao kwa kona iliyofungwa na mshikaji wake Kagere.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic