September 26, 2020




 UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo mbele ya Gwambina FC itatoa burudani na kuwapa furaha mashabiki watakaojitokeza Uwanja wa Mkapa.


Septemba 26, Simba itakuwa na mchezo dhidi ya Gwambina FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuhitaji kupata pointi tatu muhimu.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanahitaji kutoa burudani na kupata pointi tatu ndani ya uwanja.

"Tunahitaji kutoa burudani na kufanya vizuri kwenye mchezo wetu ambao tutaingia uwanjani tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tunahitaji pointi tatu.

"Viingilio ni vilevile vyenye ladha ileile 3,000 mzunguko ni kero kwenda mbele, sambusa za kwenda mbele wamesema wameongeza wachezaji kitu kingine wameahidi kuonyesha ushindani mkubwa, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

Simba inashuka uwanjani ikiwa imeshinda mechi mbili mbele ya Ihefu FC kwa ushindi wa mabao 2-1 na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United, sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar.

Gwambina FC imepoteza mechi mbili ikiwa ni ile ya ufunguzi dhidi ya Biashara United ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0,ilifungwa pia na Ruvu Shooting bao 1-0 na mechi yake ya sare ilikuwa mbele ya Kagera Sugar, ilikuwa ni sare ya bila kufungana.

3 COMMENTS:

  1. Wanakaa 4 au 5 warudi kwao mwanza haina kungoojea

    ReplyDelete
  2. Paa zahera ndio anawaponza Gwambina maana bado tunahasira nae

    ReplyDelete
  3. Zahera atawaponza kwelikweli, maana alifanya mpaka s'vital kula kichapo kitakatifu. Hao gwambina wajiandae kuwa ndo team ya kwanza kupigwa kichapo Cha mbwa koko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic