September 13, 2020


JANA  Jumamosi, Septemba 12, Simba ilibanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amemtaja mchawi ambaye anaweza kuwazuia wasiwe mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.


Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Simba ikiwa na kikosi chake kamili, ililazimishwa sare ya bao 1-1 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Mzamiru Yassin alikuwa wa kwanza kuitanguliza Simba mbele kwa bao lake dakika ya 45 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mtibwa Sugar.Mapema tu kipindi cha pili dakika ya 46, Boban Zirintusa aliisawazishia Mtibwa na kufanya matokeo kuwa 1-1.

 

Licha ya timu zote kufanya mabadiliko ya mara kwa mara, lakini hakuna timu iliyoongeza bao, hadi mwisho matokeo yakawa 1-1.


Sven msimu huu ana kazi ya kutetea ubingwa wa ligi hiyo, amesema: “Licha ya usajili bora ambao kikosi chetu kimeufanya, lakini kuna changamoto moja ambayo inaweza kutuzuia tusiwe mabingwa.


“Changamoto kubwa ambayo ninaiona tutakuwa nayo msimu huu ni ile ya kutafuta uwiano kwenye maeneo mawili ambayo ni eneo la ushambuliaji na ulinzi, naamini kama tutaweza kutengeneza muunganiko mzuri katika maeneo hayo basi naamini hakuna wa kutuzuia kutwaa ubingwa,” alisema Sven.

 

Matokeo mengine ya mechi za jana ni; JKT Tanzania 0-2 Dodoma Jiji, mabao ya Dodoma yalifungwa na Jamal Mtegeta dakika ya 50 na Dickson Ambundo (dk 80). KMC 2-1 Prisons, wafungaji wa KMC ni Hassan Kabunda dakika ya 21 na Keneth Masumbuko (dk 90), lile la Prisons lilifungwa na Kassim Mdoe dakika ya 39.


4 COMMENTS:

  1. Kcha atathmini mfumo wake anaiuhusudu kama ndio utakaompa matokeo. Kuna mifumo mingine duniani atumie mifumo tofauti tofauti kulingana na aina ya wachezaji alio nao. Kikosi kina wachezaji wazuri ila yeye mwenyewe anawaweka benchi anashindwa kuwatumia. La sivyo akiri mbinu zimeshaisha hapo ndio ukomo wake

    ReplyDelete
  2. Kwahiyo kila Team isipopata matokeo tatizo ni uwiano wa sehemu fulani? Na je Manara hilo hakulijua akawashauri Simba wasiodhurura.Sasa mimi mdhururaji kwa hii Simba mchezaji pekee walomsajili aingie moja kwa moja kwenye 1st eleven yao Ni B Morrisoni. Waliobaki inategemea walokuwepo wameamkaje.Hata yule namba mbili Duchu anaweza kucheza wamwamini cse Kapombe anakimbia kimbia hovyo hatulii.

    ReplyDelete
  3. Nawewe umeanza kutuzingua bora usepe tu.huna jipya

    ReplyDelete
  4. Coach Hana utetezi wa msingi, ila anashindwa kujua antumie mchezaji yupi kwa wakati upi, kuamini baadhi ya wachezaji hata waboronge vipi, na kushindwa kufanya sub zenye tija kwa wakati. Huwezi acha kuwachezesha Bwalya na Miraji Athuman kwa mazingira ya mechi ya Jana.
    Ajiangalie Sana vinginevyo nauona mwisho wake hata kabla ya mzunguko kwanza haujaisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic