Dakika 90 Uwanja wa Sokoine zimekamilika kwa mchezi kati ya Ihefu FC na Simba kumalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1.
Mabao yalifungwa na John Bocco dakika ya 10 na la ushindi lilifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 42.
Lile la Ihefu lilifungwa na Omary Mponda dakika ya 14 na kwa sasa Simba wamefanikiwa kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza.
Zimeongezwa dakika 3
Dakika ya 80
Uwanja wa Sokoine
Ihefu 1-2 Simba
MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kwa sasa Uwanja wa Sokoine leo Septemba 6 kati ya Ihefu FC dhidi ya Simba ni kipindi cha pili.
Ihefu wanakwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wamefungwa mabao 2-1 ambapo Simba ilianza kufunga bao kupitia kwa John Bocco dakika ya 10 lilisawazishwa na Omary Mponda dakika ya 14.
Bao la pili kwa Simba lilifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 42.
Ihefu ambayo imepanda daraja ipo kwenye ubora wake ambapo wanacheza soka la utulivu na kuwapa tabu mabingwa watetezi Simba leo.
Sio lazima uchambue moja kwa moja, Kama huwez kuweka matukio ya msingi, Kama goli kafunga Nani, dakika ya ngapi, acha tu mechi iishe uweke matokeoya jumla.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHahaaaa. Sjui anakimbilia wapi. Anaacha kutoa taarifa kamili, anatoa nusu nusu
DeleteUtafikiri kalazimishwa
ReplyDeletembona mnamuwakia sasa?
ReplyDeleteKikosi kipana kinatolewa kamasi na katimu kama ihefu? Mwaka huu mnaishia raundi ya kwanza tena CAF
ReplyDeleteTeh teh teh teh nacheka sana nikiona hii coment,we ulisikia wapi?mambo ya teofila hayo ndugu yangu pole sana.
DeleteHuyo saleh ni GONGOWAZI kwani hamjuwi?
ReplyDeleteUnazungumza ya mwenzio wakati wewe bado hujafahamu unatokaje!, mpira ni dakika 90 ndio utoe povu
ReplyDeleteMechi ipi Yanga au Azam alimfunga Ihefu??
ReplyDeleteVipi mechi yenu ya NYUMBANI matokeo yakoje?pamoja na kubebwa.