AMRI Said, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Mbeya City amefutwa kazi Oktoba 20 kutokana na timu kutokuwa na mwendo mzuri msimu wa 2020/21.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha msaidizi Mathias Wandiba ambaye ataendelea kuwa msimamizi wa timu hiyo iayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Mchezo wake wa mwisho ilikuwa jana Oktoba kukaa kwenye benchi na timu ya Mbeya City ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.
Kwa msimu wa 2020/21, Mbeya City imejenga ufalme wake nafasi ya 18 kwa kuwa imedumu kwa muda wa raundi saba mfululizo.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi saba kibindoni ina pointi mbili kwa kuwa ilipata sare mechi mbili ndani ya ligi na kupoteza jumla ya mechi tano.
Safu yake ya ushambuliaji iliweza kufunga bao la kwanza jana Oktoba 20 wakati ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.
Kila la heri uendako kaka
ReplyDeleteKila lakheri Amri, utapata team nzuri tu, hyo mbeya inashuka daraja maana Ni donda ndugu.
ReplyDeleteWamekuonea, timu Haina wafungajji
ReplyDeleteTimu mbovu kocha kafanya nini? Utapata timu ndiri kaka achana na hao na ukabila wao
ReplyDeleteTeam kimeo Ile ishuke tu daraja maana inagawa tu point, kila mtu anajipigia
ReplyDelete