October 7, 2020

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa namna kikosi chake kilivyo huwa anapata tabu kuchagua kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wa kila mchezaji ndani ya uwanja na wakiwa mazoezini.


Wachezaji ambao kwa sasa ndani ya Simba wamekuwa wakikosekana kikosi cha kwanza ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Bernard Morrisons, Erasto Nyoni, Beno Kakolanya.


Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara ambalo walitwaa taji msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kufikisha pointi 88 kibindoni wana kibarua kizito cha kupambania taji lao kutokana na ushindani uliopo kwa msimu wa 2020/21.  


Tayari imeshacheza mechi tano na kujikusanyia pointi 13 kibindoni, imeshinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa amkuwa akipata wakati mgumu kwenye kuchagua kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wa wachezaji wake.


"Ukitazama kwenye kila idara kwangu kuna wachezaji zaidi ya wanne, labda kwa mfano ukigusa upande wa washambuliaji ninao wanne ambao ni Meddie Kagere, Charlse Ilanfya, Chris Mugalu na John Bocco.


"Kila mchezaji ana uwezo na kila mchezaji anahitaji kucheza, hakuna chaguo na huwezi kuwatumia wote hivyo kwangu ni furaha kwa kuwa ninakuwa kwenye wakati mgumu huku nikiwa na wachezaji ambao wanauwezo wa kunipa matokeo.


"Kinachotakiwa ni kwa kila mmoja kupambana ndani ya uwanja ili kuonyesha uwezo zaidi ya mwingine na ninaamini wote ni bora na nitawatumia," amesema.


kwenye mechi tano ambazo amekaa kwenye benchi ameshuhudia wachezaji wake wakifunga mabao 14 na Aishi Manula mlinda mlango namba moja akiokota mipira nyavuni mara mbili.

2 COMMENTS:

  1. Wewe tulishakujua kuwa unajitungia mambo,kama siyo ufara kweli Ajibu anacheza namba sawa na MORRISON?? Pumbavuuuuuuu

    ReplyDelete
  2. Wewe tulishakujua kuwa unajitungia mambo,kama siyo ufara kweli Ajibu anacheza namba sawa na MORRISON?? Pumbavuuuuuuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic