MARIO Gotze mchezaji wa zamani wa Klabu ya Borussia Dortumud na Bayern Munich amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya PSV Eindhoven akiwa mchezaji huru baada ya dili lake ndani ya Dortmund kumeguka.
Nyota huyo mwenye miaka 28 raia wa Ujerumani ambaye aliwahi kushinda taji la Kombe la Dunia mwaka 2014 wakati timu yake iliposhinda bao 1-0 dhidi ya Argentina na mwaka huo alitupia mabao manne kwenye timu yake ya taifa.
Alikuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya AC Milan, Lazio, AS Roma na Atletico Madrid mwisho wa siku nyota huyo ameibuka ndani ya PSV
Gotze amesema kuwa alikuwa na ofa nyingi mkononi kwa msimu wa 2020/21 jambo ambalo lilimfanya ajipe changamoto yeye mwenyewe kuchagua timu ambayo ataitumia na ameamua kutua PSV kwa kuwa anaamini atakwenda sawa na falsafa zao.
'Nilikuwa nina ofa nyingi kabla ya kutua hapa na ilikuwa ni changamoto kwangu kwani kila timu iliyokuwa inanihaitaji ni bora na nilkuwa ninapenda kuitumikia lakini kwa kuwa nipo hapa basi nitapambana ndani ya changamoto yangu mpya," amesema.
John de Jong, kiongozi wa PSV kwenye benchi la ufundi amesema kuwa anaamini atakuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho hivyo atapewa ushirikiano mkubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment