October 7, 2020

 



BAADA ya uongozi wa Yanga kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Zlatko Krmpotic aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2020/21 kwa sasa mchakato wa kumpata kocha mpya unaendelea.

Tayari kikosi cha Yanga, jana Oktoba 6 kimeingia kambini na kuanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18 Uwanja wa Mkapa kuna orodha ya majina ambayo yanafanyiwa mchujo.

Miongoni mwa majina hayo ni pamoja na yale ya makocha ambao walituma maombi yao mwanzoni mwa msimu wakati walipohitaji kurithi mikoba ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji pamoja na yale ambayo yalikuwa ni chaguo la uongozi.

Haya hapa majina yanayotajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga kupokea mikoba ya Mserbia, Krmpotic aliyefutwa kazi mazima Oktoba 3:-


1.Cedric Kaze raia wa Burundi, ana leseni ya CAF, amewahi kuinoa timu ya Taifa ya Burundi, amefundisha Atletico Olimpic.


2.Geoge Lwandamina wa Zambia ana itambua falsafa ya Yanga aliwahi kuifundisha na kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.


3.Ersnt Middenorp raia wa Ujerumani ana uzoefu na soka la Afrika kwa kuwa alikuwa anainoa Kaizer Chief ya Afrika Kusini. 


4. Hans Pluijm, ana uzoefu na soka la Afrika aliwahi kuifundisha Yanga kwa mafanikio makubwa pia aliinoa Singida United na Azam FC kabla ya kufutwa kazi na ana uzoefu mkubwa.


Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga amesema kuwa mchakato unaendelea na wakati utakapofika kila kitu kitakuwa wazi.


"Wapo makocha ambao tunaangalia uwezo wao kwani huyu aliyepita licha ya kutupa ushindi kuna mambo ambayo tulikuwa tunahitaji tuliona atashindwa kutupatia.


"Miongoni mwao ni pamoja na wale ambao waliwahi kuomba kuinoa timu. Mfano Kaze ni miongoni mwa wale ambao tulikuwa tunamhitaji na kwa namna alivyo na uwezo inatosha kusema kwamba wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi." amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic