October 3, 2020


KIKOSI cha Yanga leo Oktoba 3 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Coastal Union.


 Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu ambapo hakuna timu iliyoona lango la mpinzani zaidi ya kila mmoja kuishia kupiga mashuti ambayo hayakuleta matunda.


Kipindi cha pili baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic kufanya mabadiliko kwa kumtoa Zawad Mauya nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima pamoja na kuingia kwa Deus Kaseke ambaye alichukua nafasi ya Kibwana Shomari kasi ya Yanga kushambulia iliongezeka.


Mabao ya Yanga yalifungwa na Carlos Carlinhos dakika ya 48, Haruna Niyonzima dakika ya 52 na lile la tatu lilipachikwa na Yacouba Sogne dakika 64.


Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 13 ikiwa nafasi ya kwanza na imeishusha Azam FC ambayo ilikuwa nafasi ya kwanza na pointi zake 12.

5 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Mechi tano kashinda moja nayo team yakusheherekea kumfunga 3. Lahuralakwata utopolo kadoda, kocha team imechacha hyo katafute maisha pengine penye uhai..

      Delete
  2. Gwambina kashinda ngapi kwenye ligi? Ihefu naye je?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic