KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, ameibuka na kufunguka hatma yake ya kujiunga na Yanga huku akielezea mipango yake ya kubaki kucheza Msimbazi.
Hiyo ikiwa ni siku chache kupita tangu ziwepo tetesi za staa huyo kutakiwa na Yanga inayopata jeuri ya udhamini wa GSM mara baada ya taarifa kuzagaa za kugomea kuongeza mkataba wa kuendelea kubaki Simba.
Chama ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu wa 2020/ 2021 ndani ya Simba.
Kiungo huyo amesema anafurahia maisha mazuri ndani ya Simba inayofundishwa na Kocha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.Chama alisema kuwa bado hajasaini mkataba mpya wa kuendelea kuwa Simba, lakini hivi karibuni kila kitu kitakaa sawa kwa maana ya kuongeza mkataba huo.
“Simba pana raha zaidi, hivyo ninafikiria kuendelea kubaki kuichezea Simba kwa kuongeza mkataba mwingine.
“Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu huu 2020/2021 na bado sijausaini mpya, lakini ninaamini kila kitu kitakaa sawa na nitaongeza,” alisema Chama na kuongeza kuwa:“Katika kikosi cha Simba msimu huu ninafurahia kucheza pamoja na kiungo mwenzangu Bwalya (Rarry), kwani ni kati ya viungo bora hivi sasa katika kikosi cha Simba.”
Chama ambaye msimu uliopita alitwaa tuzo mbili za kiungo bora na mchezaji bora kwenye ligi kuu, msimu huu amehusika katika mabao matano kati ya 14 yaliyofungwa na timu hiyo kwenye ligi.
Yeye amefunga mabao mawili na kutoa asisti tatu Simba ikiwa imekusanya pointi 13 kibindoni.
Hizo habari zimezagaa wapi. Au zimezagawishwa na watu wa yanga ili kuleta tension kwa simba?
ReplyDeleteJawabu ya Chama ni "raha ipo Simba" hii ina mana kuwa kule ni zogo na si pahala pa kujivunia au kuaminika
ReplyDeleteHawa waandishi wanazi wanataka kumwondoa kimawazo kwenye game wanazi wa utopolo na habari za kutunga
ReplyDeleteNguvumoja,cc hatuteteleki,acha walopoke tu
ReplyDelete