October 15, 2020


KOCHA mpya wa Yanga Mrundi, Cedric Kaze, amewatumia ujumbe mkubwa mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kwa pamoja watafanya makubwa.

Kauli hiyo aliitoa kocha huyo akiwa njiani kutua hapa nchini akitokea Canada ambapo makazi yake yalikuwa huko.


Kocha huyo anakuja kuifundisha timu hiyo baada ya kufikia makubaliano mazuri na mabosi wa Yanga akichukua nafasi ya Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyetimuliwa Oktoba 3.


Kaze amesema:-“Ninajivunia kuwa kocha mpya wa Yanga, timu yenye historia nzuri ambayo mashabiki wake ni wazuri.


“Yanga ni kati ya timu bora katika ukanda wa Afrika, kwa pamoja tutafanya makubwa, kikubwa kinachotakiwa ni ushirikiano na kupeana sapoti katika majukumu ambayo nitayaanza.


"Ninatambua kwamba kuna ushindani mkubwa ukizingatia kila timu imejipanga kufanya vizuri ili ipate matokeo chanya, ninaamini kila kitu kitakuwa sawa," amesema.

 

Kaze atatua saa nne usiku na moja kwa moja atajiunga na kambi ya Yanga iliyowekwa kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho.

9 COMMENTS:

  1. Nyie watu hamna habari nyingine za kuandika?kama mmekosa habari si vibaya mkiandika habari za mafuriko ya Dar kuliko kuchosha akili zetu kwa habari za kujirudiarudia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa nini unasoma? Hujui kuwa hii ni blog inayohusu michezo? Mbona wapo wengine wengi tu walioandika habari za mafuriko si uwafuate huko? Zinakukera sana hizi habari, ehhh?

      Delete
  2. Huyu atafukuzwa baada tu ya ya mechi tatu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utamfukuza wewe? Halafu kwanini usijishughulishe zaidi na mambo yanayokuhusu?

      Delete
  3. Huyu kaze anayesifiwa kila siku keshawahi chukua ubingwa au kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika? Kila siku kazee kazi ndo nani kiasi cha kumpa sifa zote hizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. mwambieni hata hao wsliofukuzwa walikua na matumaini mengi kuliko yy na walipokelelewa airport kwa mbwembwe

      Delete
  4. Utopoloooo wmemsajili kocha mzungu kiafrka dah!

    ReplyDelete
  5. Coach wa Yanga, wengine inawahusu nn?huo ndio ushamba mind your business

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic