October 3, 2020


 MBWANA Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC amesema kuwa wachezaji wake wakiwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma huwa wanapambana kwa juhudi zaidi kwa kuwa wapo nyumbani jambo linalowapa matokeo.

Jana, Oktoba 2 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya tano uliopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, timu ya Dodoma Jiji iliiwapapasa kwa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Mabao ya Dodoma Jiji FC yalifungwa na Jamal Mtegeta pamoja na Cleofas Mkandala na kuipa poiti tatu mbele ya Ruvu Shooting. 

Unakuwa ni mchezo wa pili kushinda kwenye uwanja wao wa nyumbani baada ya ule wa kwanza kushinda mbele ya Mwadui FC kwa kuifunga bao 1-0.


"Ukiwa nyumbani unacheza kwa kujiamini na hii inaongeza hali ya kuendelea kutafuta matokeo kwenye mechi zetu za mbele.


"Wachezaji wanapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki na wao wanalipa fadhili kwa kufanya kazi kwa juhudi ndani ya uwanja hivyo ni muhimu kila shabiki kuendelea kutupa sapoti ni kitu kizuri na kinafaa.


"Ushindi wetu ni kwa ajili ya mashabiki wetu na timu yetu tuna malengo makubwa ambayo tumejiwekea hayawezi kutimia ikiwa hakutakuwa na sapoti kutoka kwa mashabiki," amesema.

Ushindi huo unaifanya Dodoma Jiji FC kufikisha jumla ya pointi 10 kibindoni ikiwa imecheza mechi tano kwa msimu wa 2020/21 huku Ruvu Shooting ikiwa imebaki na pointi zake tano kibindoni.


Dodoma Jiji ipo nafasi ya nne kwenye msimamo na Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic