October 3, 2020


 HAROUN Mandanda mlinda mlango namba moja wa Klabu ya Mbeya City inayonolewa na Kocha Mkuu, Amri Said yupo kwenye wakati mgumu baada ya kuyeyusha dakika 360 uwanjani huku akibebeshwa jumla ya mabao saba.

 Mbeya City ikiwa imecheza mechi nne ndani ya ligi ambazo ni dakika 360 imefungwa mechi zote na safu yao ya ushambuliaji imekwama kufunga bao kwenye mechi za ligi.

Mandanda alikaa langoni wakati timu yake ikipoteza mbele ya KMC kwa kufungwa mabao 4-0 Uwanja wa Uhuru, Septemba 7 pia wakati ikipoteza kwa kufungwa na Yanga bao 1-0, Uwanja wa Mkapa, Septemba 13 alikaa langoni.


Mechi mbili za Uwanja wa Sokoine ilikua namna hii Mbeya City 0-1 Azam FC, Septemba 20, Mbeya City 0-1 Namungo FC, Septemba 25 zote Mandanda alikaa langoni jambo ambalo linamfanya awe kipa namba moja kwa wale waliofungwa mabao mengi mpaka sasa.


Mbeya City leo ina kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.


Tanzania Prisons ambao ni wageni wameibukia Sokoine wakitoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC sawa na Mbeya City ambao nao pia wamefungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic