October 15, 2020


 WIKIENDI iliyopita, ulipigwa mchezo wa kimataifa wa kirafi ki kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ilikuwa mwenyeji wa Timu ya Taifa ya Burundi. Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar, Taifa Stars ilikubali kipigo cha bao 1-0.

 

Ukiangalia taswira nzima ya mchezo ule, Taifa Stars walikuwa vizuri kwa takribani dakika 80 wakifanikiwa kuutawala mchezo, lakini umakini mdogo wa safu ya kiungo na ulinzi ukaigharimu timu kwa kufanya kosa lililozaa bao la ushindi kwa Burundi. Kabla ya hapo, safu ya ushambuliaji ilikosa mabao kadhaa.

 

Novemba 13, mwaka huu, Taifa Stars itakuwa mgeni wa Tunisia kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufunzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2022) mchezo utakaopigwa kule jijini Tunis nchini Tunisia.

 

Ukiwaangalia Tunisia ni moja ya timu bora na tishio Afrika, hivyo tahadhari kubwa kuelekea mchezo huo inatakiwa kuchukuliwa.


Benchi la ufundi la Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije na wasaidizi wake, Juma Mgunda na Seleman Matola wanapaswa kuyafanyia kazi makosa ya kiufundi yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ili kuepusha athari zaidi kwenye mchezo ujao ambao ni muhimu kwa taifa kwani ni ndoto yetu kushiriki tena michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

 

Kikosi cha stars kimesheheni nyota wenye vipaji vya hali ya juu ambao wana uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu, hivyo ni wajibu wao kujua thamani ya jezi ya timu ya taifa, mnapaswa kupambana kwa nguvu zenu zote kuhakikisha ndoto ya Watanzania inatimia kwa mara nyingine.

 

Ni jambo jema kuona Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeunda kamati ya hamasa na ushindi ambayo itasaidia kuongeza morali kwa wachezaji kujituma na kupambana uwanjani, kamati pia ihakikishe inafanya kazi yake kwa ufanisi wa hali ya juu kwani jukumu walilopewa ni kuhakikisha timu ya taifa inashinda kila mchezo.


Wachezaji mnaporudi kwenye klabu zenu hakikisheni mnafanya mazoezi na kujituma kwa hali ya juu ili mnapokuja kwenye timu ya taifa muendeleze kile mnachokifanya kwenye timu zenu.

 

Watanzania kila mmoja anatakiwa kujitoa kwa ajili ya timu ya taifa na tuungane kukemea viashiria vyovyote ambavyo vinaweza kutugawa kama taifa, utofauti ubaki kwenye klabu mnazozisapoti, lakini linapokuja suala la timu ya taifa tuhimize umoja wetu.

 

Mamlaka husika zinapaswa kuwaandalia mazingira bora wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya Tunisia ili kuwaongezea morali ya kupambana kwenye mchezo huo mgumu kutokana na aina ya timu nambayo tunakutana nayo.


Linapokuja suala la wachezaji kuingia kambini pia wanapaswa kuwahi ili kutochelewesha program za mwalimu.Kwa upande wa kocha mkuu aendelee kufuatilia mechi mbalimbali za ligi tofauti ili kupata wachezaji wenye ubora ambao watapambana kwa ajili ya taifa hapo Novemba 13 kule Tunisia.

 

Tukumbuke kuwa, Taifa Stars ipo Kundi J, baada ya kucheza mechi Novemba 13 dhidi ya Tunisia, timu hizo zitarudiana Novemba 17, mwaka huu jijini Dar. Tunahitaji kufanya vizuri, hivyo tushirikiane.

4 COMMENTS:

  1. Mkubwa kuwapa moyo Wachezaji Ni vizuri ,hapa Kuna tatizo la Ukweli lazima tuambizane ,hata Mechi ya juzi dhidi ya Burundi mchezaji pekee mwenye Kiwango sawa na Burundi Ni Samatta ,najua wengi tunaangalia kukimbia na kupigiana vipasi visivyo advance .Kwa Tunisia tutachapwa Tena hapo tutakapokwenda na ujuaji wetu wa kupiga pasi.Na Nina shauri Wachezaji wa Simba wawe wachache cse wao wao wamezoea kuzidi Timu pinzani wanapozidiwa wanachemka wapangwe watatu tu mkibishi mtanikumbuka.na tujue Tunisia siyo level yetu matokeo yoyote tuyapokee

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kulikuwa na wachezaji wangapi wa Simba walivyocheza na Burundi?Tatizo la wabongo kila mtu kocha...

      Delete
  2. Ndemla alikuwa anatafuta nini mle? msimu ulopita hakucheza mkawa mnasema atafute changamoto kwingine , kucheza tu Mechi mbili nazo hamalizi anaitwa National Timu Tena anaanza,nashauri hata Matola atoke benchi la ufundi.

    ReplyDelete
  3. Simba inawachezaji wanne wa uhakika National Team .Manula, Kapombe (50/50),Mkude na Bocco lkn mlivyouteka mpira wetu kwa parojo utaona mala Miraji Athumani,Mohd Hussein,Mzamiru hata Kennedy Juma Hawa Ni wachezaji wa kawaida Kama walivyo wa Prison,Mtibwa nk ndiyo maana mkiwafunga mnashangilia Sana mkisahau hizo Timu zinazo watoa jasho Wachezaji wao wote Ni local na Wanacheza regularly huku wa Simba wengi hukaa benchi huku wakitamba Foreigners.Halafu unawaita National Timu?au pana agenda Kama siasa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic