ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amefunguka kuwa, katu wasitokee watu wa kuicheka Yanga kutokana na ushindi wa bao moja katika kila mechi kwani wana uwezo wa kutwaa ubingwa kwa mabao hayohayo msimu huu.
Yanga ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwa kushinda michezo mitatu kati ya minne iliyocheza kutokana na kutoa sare dhidi ya Tanzania Prisons, imejikuta ikipata ushindi wa bao moja katika kila mchezo.
Rage ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT sasa TFF, amesema kuwa, Ligi ya safari hii ni ngumu na ina ushindani mkubwa kutokana na kila timu kufanya usajili mzuri, hivyo kusitokee mtu akabeza matokeo ya timu fulani.
“Ligi ni ngumu, kuna ushindani wa hali ya juu, timu zimejitahidi kufanya usajili mzuri na wachezaji wote wana majina hususani Simba na Yanga, hivyo kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.
“Hivyo asitokee mtu akabeza matokeo ya timu fulani, watu wanasema Yanga inashinda lakini mabao machache inapata bao moja katika kila mechi, wanaweza wakatwaa ubingwa na ushindi huohuo wa bao moja kwani hata Ulaya kuna timu ilitokea ilipata ubingwa kwa ushindi wa bao moja hivyohivyo hadi mwisho wa msimu, hivyo kila timu ipambane,” alisema Rage.
Chanzo:Championi
Sawa mzee
ReplyDeleteHakiwezekani asilani
ReplyDeleteHakika yote yanawezekana
ReplyDeleteDUH HIYO NI KALI JAPO INAWEZEKANA KUTOKANA NA MAONI YA RAGE ILA MASHABIKI WAJIANDAE KISAIKOLOJIA BAADA YA LIGI KUFIKIA TAMATI WENGI WAO WATAKUBWA NA MARADHI YA PRESHA MANA JAMAA MATCH YAO IKIANZA KUANZIA DAKIKA YA 1 HADI 90 NI FULL PRESHA KWA MASHABIKI WAKIDHANI MUDA WOWOTE WANASAWAZISHIWA
ReplyDeleteWABADILI MTAALAM WA KAMATI ISIYOJULIKANA ILI ANGALAU WAFUNGE HATA KUANZIA BAO 2, KWA NJIA NYINGINE WAZEE WA MIKEKA WAMERAHISISHIWA
ReplyDeleteYANGA ACHENI KABISA HIYO TABIA YA MIKIA KUNUNUA MECHI. KWANZA NYIE HAMJAKOPWA CHOCHOTE. ACHENI TIMU IPAMBANE WANJANI
DeleteYANGA ACHENI KABISA HIYO TABIA YA MIKIA KUNUNUA MECHI. KWANZA NYIE HAMJAKOPWA CHOCHOTE. ACHENI TIMU IPAMBANE WANJANI
Delete