October 30, 2020

 


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wapambane na kila mchezaji atakayekuwa na jezi ya njano uwanjani bila kujali uwezo wake upoje ndani ya uwanja.


Kesho, Oktoba 31 Biashara United iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 16 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 19.


Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo vizuri na wanaamini kwamba watapata matokeo kwenye mchezo wa kesho.


"Nimewaambia wachezaji kwamba wana jukumu la kuambana na kila mchezaji mwenye jezi ya njano ndani ya uwanja bila kujali uwezo wa wapinzani wangu.


"Ni wacheche kwa sasa ambao wamefungwa mabao machache ndani ya ligi ambao ni Yanga sasa kazi kubwa itakuwa kwenye kusaka ushindi hilo lipo wazi lakini tutapambana," amesema.


Safu ya ulinzi ya Yanga imeruhusu mabao mawili ya kufungwa ndani ya ligi ikiwa imecheza jumla ya mechi saba huku ile ya Biashara United ikiwa imeruhusu kufungwa mabao saba baada ya kucheza mechi nane.

3 COMMENTS:

  1. Tatizo marefa,mnaweza kuwamudu yanga ila muamuzi akatoa penati

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwamuzi wa yanga na kmc kaambiwa aongeze umakini wakati waamuzi wengine waliovurunda wamepewa adhabu

      Delete
    2. Aliyekwambia penati goli akamuulize Bocco

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic