October 6, 2020

 


MUDA mfupi kabla ya kusitishiwa mkataba wake ndani ya Yanga, Oktoba 3, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic alisema kuwa sababu kubwa iliyomfanya asimtumie mchezaji Haruna Niyonzima kikosi cha kwanza ni utomvu wa nidhamu.

Krmpotic  alikiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara ambazo ni dakika 450 na alishinda mechi nne huku akilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mechi tano za ligi ambazo Krmpotic alikuwa kwenye benchi, Niyonzima alianza kikosi cha kwanza mechi moja mbele ya Mbeya City na alitumia dakika 69,mechi mbili hakucheza mbele ya Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar .

Mechi mbili alianzia benchi ilikuwa mbele ya Kagera Sugar alitumia dakika 7 na mbele ya Coastal Union alitumia dakika 45, jumla Niyonzima ametumia dakika 121 kati ya 450 akikosekana kwenye dakika 329.

Krmpotic alisema:”Haruna Niyonzima ni mchezaji mzuri ila ana mambo yake ambayo yalikuwa ni nje ya uwanja, mfano kabla ya mechi yetu dhidi ya Coastal Union kuna siku mbili alichelewa kurudi kambini ikiwa ni pamoja na Jumatatu, sasa hapo ilikuwa ngumu kumuanzisha moja kwa moja kikosi cha kwanza.”



10 COMMENTS:

  1. kocha yupo sahii sema viongozi wetu wanwaogopaga wachezaji sana

    ReplyDelete
  2. ana nidhamu sana tu.kocha mwenyewe ndo hakuwa na nidhamu ndo maana kaondoka

    ReplyDelete
  3. Kwa watu wasiomjua vizuri Niyonzima watamtetea sana lakini kwa mashabiki na wanachama wa Yanga tulio karibu na wachezaji na benchi la ufundi tunaijua vizuri tabia yake.Yeye ni mmojawapo wa lile genge la wahujumu ambao walikuwa wanatumiwa na makofia na mwenzake kupokea na kugawa mlungula kwa wengine ili timu ifungwe.Ilifikia hatua walikuwa wanawekeana vinyongo kwa sababu ya kiasi gani mtu alikuwa amepokea.Niliwahi ku comment humu kama ingekuwa ni maamuzi yangu wala asingesajiliwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli, kati wachezaji waliobaki, Haruna ni kirusi. Anajivuna na kujiona anajua saana. Huchagua mechi na ni kinara wa ugomeshaji!
      Mwenzie Yondani na Juma wameachwa, mkataba wake ukiisha asepe

      Delete
    2. Makofia ndio nani tena?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic