October 15, 2020


IMEELEZWA kuwa nyota wa Klabu ya Azam FC, Prince Dube ameingia kwenye anga za Klabu ya Raja Casablanca ambayo inahitaji kuinasa saini yake.


Casablanca inapigana vikumbo na Klabu ya Simba ambayo nayo inatajwa kumpigia hesabu Dube.


Ofa ya Casbalanca inatajwa kuwa ni nono hivyo ikwa itawekwa mezani Simba ina kazi ya kujipanga kupindua dili hilo.

  Ofisa Habari wa Simba hivi karibuni alisema kuwa miongoni mwa nyota ambao wanaweza kupambania namba ndani ya Klabu ya Simba kutoka ni pamoja na Dube ambaye ni kinara wa utupiaji.


Ametupia mabao matano na ana pasi mbili za mabao zote alimpa mshikaji wake Obrey Chirwa.


Ofisa Habari wa Azam FC ambaye amekuwa na ushirikiano mkubwa na vyombo vya Habari, Zakaria Thabit amesema kuwa hizo ni tetesi tu.

12 COMMENTS:

  1. Simba wanaomba msaada Azam please wasaidieni Kama kawaida yenu,maana mmezoea nafasi ya tatu,.Mnaiweka Yanga mtu Kati bt this time Ni Kati ya Azam au Simba nafasi ya pili na ya tatu.Na tahadhari kwenu Azam mnafanywa Kama Pamba ya Mwanza mtakuja kushuka daraja,ilifika wakati 1st eleven ya Simba yote Kama siyo 3/4 ilikuwa Pamba.Na ninyi toka muwape wale Wachezaji wanne Ni miaka mitatu wamekuwa mabingwa mfululizo hata Lile kipindi Cha kuchukua Wachezaji Pamba walitamba.Mimi nawashangaa Azam nguvu wanayotumia kubomoa na kushindana na Yanga,huku Yanga ikiwaza kuondoa Simba kileleni ,Azam anawaza kuizidi Yanga huku ikijilegeza mbele ya Simba..Shangaaa kwa Timu zote zilizomaliza Top five hapana Timu hata moja ilichukuliwa Pointi sita na Simba zaidi ya Azam,na Simba wanajua hata mwaka huu wanazo pointi sita kwa Azam
    Sasa Azam hii Yanga ya Carlinho siyo ya Moringa Ina lake jambo so huo unazi mnaonyesha kwenye Azam TV kuwa Pamba Simba endeleeni kuwabeba hata Uwanjani kwa kujilegeza hasa kupanga kikosi hafifu sisi Wananchi this time tutawabaka wote mtake msitake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inaelekea kichwa chako hakiko sawasawa. Hivi Azam atambeba Simba kwa kitu gani? Wewe subiri kipigo kitakatifu hapo Nov 7 ndio utajua Mnyama si timu ya mchezo mchezo

      Delete
    2. Pumba tupu sijui mnakula maharage ya sampuli gani?

      Delete
  2. Kila timu ipambane na hali yake, walikuwepo toto.... wako wapi sasa

    ReplyDelete
  3. Simba akacheze nafasi ya nani hana namba pale simba acheni kukuza mambo,mechi tano tu kelele mingi

    ReplyDelete
  4. Azam ni academy ya Simba wachezaji wako on Transit kwenda Simba

    ReplyDelete
  5. Azam ni academy ya Simba wachezaji wako on Transit kwenda Simba

    ReplyDelete
  6. Azam ni academy ya Simba wachezaji wako on Transit kwenda Simba

    ReplyDelete
  7. Wewe Simba akacheze nafasi ya Nani? Kama Yale maviziaji yanafunga sembuse huyo mtaalamu,najua utaanza kusikia eti Popat Simba mwenzenu atatusaidia tumpate hapo mmenoa,ila mkubali Azam wanawabeba mno na wanapenda kuwa weaken Yanga for the sake of kutafuta machozi Simba.Angalia story ya Kavumbagu,Damayo,Ngoma na Chirwa utanielewa.Kipindi hicho Mikia bado Mo alikuwa anazichanga za misiba na maji mlikuwa hoi Azam wakawa wanawabeba.Maana toka walipozuia mchele mbovu aliishiwaga.Sasa karudi lkn mnavizia waliokosewa mikataba cse Lage yupo atawasaidia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkiambiwa akili zenu kama yule mnyamma mnakasirika huyo Dube ana utaalamu gani? wa kuizuzua Simba, mechi nne tu alizocheza Chamazi ndo aizuzue kwa kuwa nyie Chura fc mmeshazoea kuchukua wachezaji wa magazetini mnajua simba nao watatababaika bure kabisa.

      Delete
  8. Utopolo wachezaji wngp tuliowapatia.

    ReplyDelete
  9. Hakuna sehemu yoyote ambayo Raja Casablanca wameonesha nia ya kumtaka huyo Dube hayo ni magazeti ya Bongo yanampamba, kwa kitu gani hasa alichokifanya acheni kuwaongopea watu eti dola milioni 1 mnavyoitamka kirahisi hakuna mchezaji wa Azam anaweza kuuzwa bilioni mbili. Yaani kazifunga sijui Mwadui , ihefu ndo auzwe kwa bilioni haingii akilini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic