October 16, 2020


KIKOSI cha Azam FC kimeendeleza moto wake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kushinda mechi sita mfululizo na kujiwekea kibindoni pointi 18.


Kikiwa chini ya Aristica Cioaba kimecheza mechi sita za Ligi Kuu Bara na kushinda zote huku kikifunga jumla ya mabao 12.

Ushindi wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex unaifanya timu hiyo kuwa tishio ndani ya Bongo kwa msimu huu kikizipoteza timu zote zinazoshiriki ligi.


Ni Azam pekee ambayo haijapoteza mchezo wake wala kuambulia sare ambapo Simba imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons. 

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kutwaa ubingwa wa ligi jambo linalowafanya wazidi kupambana muda wote.

Mabao ya Azam FC jana yalifungwa na Obrey Chirwa aliyetupia mabao mawili dakika ya 28 na 63 huku kinara wa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara Prince Dube akitupia bao lake la sita dakika ya 61.


 Mabingwa watetezi Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao 14.

1 COMMENTS:

  1. Ubingwa msahau tusubiri mzunguko wa kwanza uishe huu ufalme ni wa timu mbili mwaka huu,wakikutana na yanga,simba na Kmc ndio tutawakubali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic