LICHA ya mzawa Yusuph Mhilu kufikisha idadi ya mabao matatu ndani ya Kagera Sugar jana Oktoba 14, timu yake iliyeyusha pointi tatu baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara raundi ya sita ulichezwa Uwanja wa Majaliwa. Mabao ya Namungo yalifungwa na Hashim Manyanya pamoja na Bigirimama Blaise ambaye naye anafikisha mabao matatu ndani ya ligi.
Kagera Sugar inazidi kuwa na mwendo wa kusuasua kwa kuwa mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex.
Mhilu amekuwa na mwendo mzuri wa kucheka na nyavu kwa wazawa ambapo rekodi yake inaonyesha kuwa mechi zote tatu alizoanza ndani ya uwanja ametupia.
Alianza kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC kisha ikafuata Kwenye kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya Azam FC na jana Oktoba 14 dhidi ya Namungo FC.
Wangeshuks daraja muda tu Hawa Zama zao zishaisha, sasa wanagawa point.
ReplyDelete