MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Tanzania, Mbwana Samatta anatarajiwa kuwasili nchini kesho kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa na mechi ya kifariki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi itakayochewa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Samatta aliyefunga mabao yote mawili ya ushindi ya Fernebahce dhidi ya Fatih Karagumluk katika mechi ya ligi kuu nchini Uturuki iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ikumbukwe timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars inaingia kambini leo Oktoba 5, huku baadhi ya wachezaji walioitwa na kocha Etienne Ndayiragije wamewasili kambini leo Oktoba 5 kujiwinda na mchezo huo.
Wachezaji wengine wa kimataifa ni pamoja na Thomas Ulimwengu anayetarajiwa kuwasili leo akitokea Congo DR, Himid Mao, Simon Msuva na Nickson Kibabage kutokea Misri na Morocco watawasili Jumatano naye Ally Msengi tayari amewasili akitokea Afrika Kusini.
Etienne Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa.
0 COMMENTS:
Post a Comment