October 3, 2020

 


HUKU kukiwa na fukuto la  mkataba wake likiwa limeanza upya ndani ya klabu yake ya zamani ya Yanga wakidai kuwa mkataba wake ni batili ndani ya Simba, rekodi zinaonyesha kuwa kiungo Bernard Morrison amepotezwa jumlajumla na Carlos Carinhos wa Yanga kwa upande wa pasi za mwisho.

Ndani ya dakika 137,Carinhos amempoteza Morrison kwa upande wa pasi za mwisho ambapo yeye ni kinara ndani ya Yanga akiwa nazo mbili huku Morrison akiwa na pasi moja ya bao ndani ya dakika 181.

Ujanja wa Morrison ni Uwanja wa Mkapa ambapo pasi yake ya kwanza ndani ya ligi akiwa Simba alimpa Chris Mugalu wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC huku Carinhos akipeta kwa Mkapa kwa kumpa pasi Lamine Moro kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na pasi ya pili alitoa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

Carinhos amepiga jumla ya kona 11 ambapo alipiga kona 5 mbele ya Mbeya City kona 2 mbele ya Kagera Sugar na kona 4 mbele ya Mtibwa Sugar na katika hizo kona mbili zilisababisha mabao Morrison alipiga kona 3 mbele ya Ihefu na kona moja mbele ya Gwambina FC akiwa amepiga jumla ya kona nne hakuna hata moja iliyoleta bao.

 Mechi za Carinhos ilikuwa:-  Mbeya City dk 30 Uwanja wa Mkapa,Kagera Sugar dk 35 Uwanja wa  Kaitaba dk 72 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa  Jamhuri.

 Morrison alitumia dk 67 mbele ya  Ihefu Uwanja wa Sokoine, dk 66 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, dk 25 mbele ya Biashara na dk 23 mbele ya Gwambina zote Uwanja wa Mkapa.


3 COMMENTS:

  1. Ushabiki utawaumiza hasa mwaka huu, Morrison wa kumfananisha na Carinhos!!

    ReplyDelete
  2. Huyu mwandishi anafanya makusudi ili apate viewers wengi anajua washabiki wengi wanaoingia mtandaoni ni wa simba simb maana anajua akiandika habari ya uongo kuhusu Simba watu wengi watacomment dawa ninkumkaushia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic