October 14, 2020

 


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo amefunguka kuwa Yanga ina bahati kubwa ya kuweza kumnasa kocha Cedric Kaze kwa kuwa anaamini sasa wanaweza kucheza soka la pasi katika uwanja wowote wataokwenda kucheza kutokana na kocha huyo kuwa na utalaam huo.

 

Mavugo ametoa kauli hiyo kufuatia uongozi wa Yanga kumalizana na Kaze ambaye anakuja kubeba mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic, aliyesitishiwa kibarua chake.

 

Kaze anatarajiwa kuingia Afrika Mashariki kesho akitokea Canada kabla ya kumalizana na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kuanza kazi. 


Mavugo amesema:- “Unajua shida ya nchi zetu zipo kwenye viwanja ambavyo vingi vimekosa ubora wa kutosha lakini bado naamini Yanga wataona faida ya kuwa na Kaze kwa sababu timu itaweza kucheza soka la kuvutia kwa pasi nyingi katika uwanja wowote ambao watakwenda.


 

“Uzuri nimecheza hapo na naelewa lakini nimefanya kazi na kocha Kaze wakati nilipokuwa Atletico, naongea kitu ambacho nakijua juu yake lakini yeye mwenyewe siyo mgeni na mazingira ya Tanzania pamoja na mpira wake, hivyo mashabiki wa Yanga watarajie makubwa kutoka kwake,” alisema Mavugo.

2 COMMENTS:

  1. Timu zetu hizi huwa zinapata makocha wazuri sana ila tatizo sijui ni wachezaji wetu au mfumo kuwa rafiki na wachezaji kwa hiyo kaze naye ni wale wale akikaa miaka miwili ni bahati!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic