October 14, 2020

 MECKY Maxime,  Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa uhakika wa kusepa na pointi tatu mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. 



Leo Oktoba 14, Kagera Sugar inajitupa Uwanja wa Majaliwa kusaka pointi tatu muhimu ikiwa ni mzunguko wa sita baada ya ule wa tano kukamilika.


Timu zote zinakutana uwanjani zikiwa na matokeo yanayofanana kwenye mechi zao zilizopita ambapo Kagera Sugar wageni wametoka kutunguliwa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex huku wenyeji wao Namungo wakitoka kutunguliwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Majaliwa.


Maxime amesema:"Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa ila tupo tayari kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja, mashabiki watupe sapoti."


Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara,  Kagera Sugar ipo nafasi ya 13 na pointi 4 inakutana na Namungo iliyo nafasi ya 9 na pointi 6.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic