KINARA wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara, Prince Dube amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyopenda ndani ya ardhi ya Bongo ni ukarimu wa Watanzania pamoja na chai na chapati kwa upande wa misosi.
Raia huyo wa Zimbabwe amekuwa na ushkaji mkubwa na nyavu huku nyota yake na mshambuliaji namba moja wa Azam FC, Obrey Chirwa ikionekana kukubali.
Akiwa amefunga mabao matano ndani ya Ligi Kuu Bara na pasi mbili za mabao, zote amempa Chirwa Uwanja wa Azam Complex jambo linalodhihirisha pacha yao kujibu.
Dube amesema:" Nafurahi kuwa hapa Tanzania, ujue watu wake ni wakarimu na wanapenda mpira jambo ambalo linanipa raha na furaha pia kila wakati.
"Mbali na hilo kwa upande wa chakula ninapenda kula chapati na chai ni aina ya chakula ambacho huwa ninakipendelelea mno pamoja na uji wakati wa jioni ni mzuri."
Timu ya Azam FC ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 15 imecheza mechi 5 na kusepa na pointi tatu zote kwenye mechi hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment