October 29, 2020


 JONAS Mkude, kiungo mkabaji wa muda mrefu ndani ya Simba ambaye ana uhakika wa namba kikosi cha kwanza amesema kuwa kwa sasa timu hiyo inapitia kwenye kipidi kigumu kutokana na aina ya matokeo ambayo wanayapata.


Simba imepoteza mechi mbili mfululizo ndani ya ligi ambazo ni dakika 180 na kuifanya ibaki na pointi zake 13 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.


Ilipokea kichapo cha kwanza msimu wa 2020/21 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.


Mkude amesema kuwa kutokana na matokeo ambayo wanayapata kwa sasa wapo kwenye kipindi kigumu jambo ambalo wanaliacha mikononi mwa benchi la ufundi.


"Matokeo magumu ambayo tunayapata kwetu ni magumu, na tunapitia kipindi kigumu kweli kwa sasa licha ya kupambana kusaka matokeo.


"Tukiwa ndani ya uwanja tunacheza kwa juhudi kusaka matokeo ila kinachotokea ni makosa na hapo ninaamini kwamba kocha anaona makosa yetu na anayafanyia kazi.


"Ninajua kwamba mashabiki wanaumia kwa sasa hata sisi pia tunaumia hivyo tunaamini kwamba mambo yatakuwa vizuri hapo baadaye," amesema.


Mchezo ujao kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi ni dhidi ya Mwadui FC unatarajiwa kuchezwa Oktoba 31, Uwanja wa Uhuru.

4 COMMENTS:

  1. Tupo nyuma yenu pambaneni mtetee ubingwa wetu maana kuna mijitu inakesha ikiomba tuendelee kufanya vibaya tuvurugane ili wapate upenyo Wa kutwaa ubingwa kirahisi, nawaambia washindwe na walegee ubingwa ni mali yetu wanamsimbazi. Kazeni majemedari wetu tupo nyuma yenu kuwasapoti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani ninyi hamuiombei Yanga Matokeo mabovu ili mchukue ubingwa? Kumbukeni kuimba ni kupokezana; na hamuwezi kuimba pekeyenu na wengine wanazo saut za kuimba

      Delete
  2. Wacheza wazawa wengi hawajitumi wanapopewa nafasi,mpaka tunatamani akina Chama Na Kagere wawepo,wana Homa za vipindi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic